Skip to content
قٓ /

Aya 7

50 : 7

Aya 7 of قٓ (50 : 7). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

قٓ Aya 45
Sura · قٓ
Kiswahili · Barawani
50 : 7

وَٱلۡأَرۡضَ مَدَدۡنَٰهَا وَأَلۡقَيۡنَا فِيهَا رَوَٰسِيَ وَأَنۢبَتۡنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوۡجِۭ بَهِيجٖ

Na ardhi tumeitandaza na tukaiwekea milima, na tukaiotesha mimea mizuri ya kila namna.

Explanation & meanings · 1
  1. Na ardhi tumeikunjua na tukaisimamisha milima iliyo kaa imara na kuthibiti kwenda chini. Na tukaijaalia kumea kila namna ya mimea mizuri ya kuwafurahisha watazamao. Gamba lilio funika ardhi katika mwahali maalumu limetuna, ndio hiyo milima. Na pengine limedidimia ndio sakafu ya chini ya bahari. Na uzani wa vitu hivi vizito vinalingana wenyewe kwa wenyewe. Na ni katika uwezo wa Mwenyezi Mungu na hikima yake kupatikana kulingana huku kwa uzani, na ukawa umethibiti kwa kupenya madda za ardhi zilizo fanyika hilo gamba jembamba chini ya mat'abaka ya juu juu. Na hayo ni kutoka kuliko kuwa kuzito kwendea kuliko kwepesi.