Skip to content
البَقَرَة /

Aya 183

2 : 183

Aya 183 of البَقَرَة (2 : 183). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

البَقَرَة Aya 286
Sura · البَقَرَة
Kiswahili · Barawani
2 : 183

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُتِبَ عَلَيۡكُمُ ٱلصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ

Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu.

Explanation & meanings · 1
  1. Na kama tulivyo kuwekeeni sharia za Kisasi na Wasiya kwa ajili ya maslaha ya jamii zenu, na kuhifadhi mambo ya ukoo, kadhaalika tumeweka sharia za Saumu ili kuzitengeneza nafsi zenu, ziweze kujikinga na matamanio, na kukutukuzeni kuliko wanyama walio baki wanao fuata hisiya za matamanio yao tu. Na huku kufaridhishwa Saumu ni kama walivyo faridhishwa kaumu zilizo tangulia. Basi msilione kuwa ni jambo zito mno hili, kwani watu wote walilazimishwa haya. Kulazimishwa Saumu ni kwa ajili ipate kuleleka roho ya uchamngu, na ili muwe watu madhubuti, na nafsi zenu ziongoke sawa.