Skip to content

Swali: 22- Unafiki ni nini na ni zipi aina zake?

الباب / الفصل
قسم العقيدة

السؤال

Swali: 22- Unafiki ni nini na ni zipi aina zake?

س٢٢: ما هو النفاق وأنواعه؟

الجواب

Jawabu:

  1. Unafiki mkubwa: Nao ni kuficha ukafiri na kudhihirisha imani.

Na huu unamtoa mtu katika uislamu nao ni katika ukafiri mkubwa.

Amesema Allah Mtukufu:

"Hakika wanafiki watakuwa katika tabaka la chini kabisa motoni na wala hawatompata yeyote wa kuwanusuru"

[Suratun Nisaa: 48]

  1. Unafiki mdogo:

Kuongopa na kutotimiza ahadi na kufanya hiyana katika amana.

Na huu haumtoi mtu katika uislamu, nao ni katika madhambi na mfanyaji anajitia katika adhabu.

Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na Amani ziwe juu yake.

"Alama za Mnafiki ni tatu: Anapozungumza husema uongo, na anapoahidi huenda kinyume, na akiaminiwa hufanya hiyana".

Ameipokea Bukhari na Muslim.

ج:1. النفاق الأكبر: وهو إبطان الكفر وإظهار الإيمان.

ويُخرِجُ من الإسلام وهو من الكفر الأكبر.

قال تَعَالَى:

﴿إِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ فِي ٱلدَّرۡكِ ٱلۡأَسۡفَلِ مِنَ ٱلنَّارِ وَلَن تَجِدَ لَهُمۡ نَصِيرًا﴾

[النساء: ١٤٥].

  1. النفاق الأصغر:

مثل: الكذب، وإخلاف الوعد، وخيانة الأمانة.

ولا يُخرج من الإسلام، وهو من الذنوب، وصاحبه معرَّض للعذاب.

قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:

«آية المنافق ثلاث: إذا حدث كذب، وإذا وعد أخلف، وإذا اؤتمن خان»

رواه البخاري ومسلم.