Skip to content
Orodha ya Sura /

الزَّلزَلة

الزَّلزَلة is chapter 99 of the Quran and has 8 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

8 Aya Sura Na. 99
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

إِذَا زُلۡزِلَتِ ٱلۡأَرۡضُ زِلۡزَالَهَا

Itakapo tetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake!

Explanation & meanings · 1
  1. Ikitisika ardhi kwa mtikiso mkubwa, na ikasukika kwa ukomo wa kutisika na kusukika kunako mkinika na ikaweza kuchukua!

وَأَخۡرَجَتِ ٱلۡأَرۡضُ أَثۡقَالَهَا

Na itakapo toa ardhi mizigo yake!

Explanation & meanings · 1
  1. Na ardhi ikatoa yote yaliomo katika ndani ya tumbo lake, ikiwa khazina au maiti walio kwisha zikwa!

وَقَالَ ٱلۡإِنسَٰنُ مَا لَهَا

Na mtu akasema: Ina nini?

Explanation & meanings · 1
  1. Na binaadamu akasema kwa kushtuka na khofu: Ardhi hii ina nini hata inatikisika hivi, na inatoa vilivyomo tumboni mwake, ndio Saa imefika?

يَوۡمَئِذٖ تُحَدِّثُ أَخۡبَارَهَا

Siku hiyo itahadithia khabari zake.

Explanation & meanings · 1
  1. Siku hiyo ardhi itamsimulia mtu khabari zake zilio mshitua,

بِأَنَّ رَبَّكَ أَوۡحَىٰ لَهَا

Kwa sababu Mola wake Mlezi ameifunulia!

Explanation & meanings · 1
  1. Kwani Mlezi wake na Muumba wake atakuwa kaifunulia, kaipa Wahyi, na kaiamuru itetemeke na ijisuke suke, ndio ikafanya upesi kutekeleza amri.