Skip to content
Orodha ya Sura /

العَاديَات

العَاديَات is chapter 100 of the Quran and has 11 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

11 Aya Sura Na. 100
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلۡعَٰدِيَٰتِ ضَبۡحٗا

Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua,

Explanation & meanings · 1
  1. Ninaapa kwa farasi wa Jihadi wendao mbio, na huku pumzi zao zinasikilizana kwa sauti inayo itwa "Dh'abh'an".

فَٱلۡمُورِيَٰتِ قَدۡحٗا

Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini,

Explanation & meanings · 1
  1. Na kwa farasi hao ambao hutoa cheche za moto zinapo gonga kwato zao kwenye ardhi wanapo kwenda.

فَٱلۡمُغِيرَٰتِ صُبۡحٗا

Wakishambulia wakati wa asubuhi,

Explanation & meanings · 1
  1. Na kwa farasi hao wanao washambulia maadui asubuhi kabla jua halijachomoza;

فَأَثَرۡنَ بِهِۦ نَقۡعٗا

Huku wakitimua vumbi,

Explanation & meanings · 1
  1. Wakatimua mavumbia mengi, farasi hao, kati ya makundi ya maadui!

فَوَسَطۡنَ بِهِۦ جَمۡعًا

Na wakijitoma kati ya kundi,

Explanation & meanings · 1
  1. Ikawa vumbi limewagubika maadui hata wakaingiwa kiwewe na kufazaika.