Skip to content
Orodha ya Sura /

المُزمل

المُزمل is chapter 73 of the Quran and has 20 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

20 Aya Sura Na. 73
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡمُزَّمِّلُ

Ewe uliye jifunika!

Explanation & meanings · 1
  1. Ewe uliye jigubika kwa nguo zako!

قُمِ ٱلَّيۡلَ إِلَّا قَلِيلٗا

Kesha usiku kucha, ila kidogo tu!

Explanation & meanings · 1
  1. Inuka kwa ajili ya Swala usiku kucha, ila kidogo tu!

نِّصۡفَهُۥٓ أَوِ ٱنقُصۡ مِنۡهُ قَلِيلًا

Nusu yake, au ipunguze kidogo.

Explanation & meanings · 1
  1. Simama nusu ya usiku, au punguza kidogo katika hiyo nusu mpaka ifikie thuluthi,

أَوۡ زِدۡ عَلَيۡهِ وَرَتِّلِ ٱلۡقُرۡءَانَ تَرۡتِيلًا

Au izidishe - na soma Qur'ani kwa utaratibu na utungo.

Explanation & meanings · 1
  1. Au zidisha kwenye nusu mpaka ifikie thuluthi mbili. Na soma Qur'ani kwa pole pole ukibainisha harufi, na pa kusita usite, pasiwe na nuksani yoyote.

إِنَّا سَنُلۡقِي عَلَيۡكَ قَوۡلٗا ثَقِيلًا

ka Hakika Sisi tutakuteremshia uli nzito.

Explanation & meanings · 1
  1. Ewe Mtume! Hakika Sisi tutakuteremshia Qur'ani yenye kukusanya amri, na makatazo, na takalifu nzito nzito.