Skip to content

Swali: 10- Ni zipi aina za Tauhidi?

الباب / الفصل
قسم العقيدة

السؤال

Swali: 10- Ni zipi aina za Tauhidi?

س10: ما أنواع التوحيد؟

الجواب

Jawabu: 1- Tauhidur rubuubiya (Tauhidi ya ulezi) Nayo ni kuamini kuwa Mwenyezi Mungu ndiye muumbaji, mgawa riziki Mmiliki na mpangiliaji, yeye pekee asiye na mshirika wake.

  1. Tauhidul uluuhiyya (Tauhidi ya uungu): Nayo ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu kwa ibada, asiabudiwe yeyote ila Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  2. Tauhidul Asmaai wasswifaati (Tauhidi ya majina na sifa): Nayo ni kuyaamini majina na sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu zilizokuja katika kitabu cha Mwenyezi Mungu na mafundisho ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-, bila kupiga mfano wala kushabihisha wala kupotosha.

Na ushahidi wa aina hizi tatu za tauhidi: Ni kauli yake Mtukufu:

«Yeye Ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wa mbingu na ardhi na vilivyomo baina yake, Ndiye Mmiliki, Muumba na Mwendeshaji wa hivyo vyote, basi muabudu Yeye Peke Yake, ewe Nabii, na uvumilie katika kumtii, wewe na waliokufuata, Hana mfano Wake kitu chochote katika dhati Yake, sifa Zake na vitendo Vyake.»

[Suratu Mariam: 65].

ج:1. توحيد الربوبية: وهو الإيمان بأن الله هو الخالق الرازق المالك المدبر، وحده لا شريك له.

  1. توحيد الألوهية: وهو إفراد الله بالعبادة، فلا يعبد أحد إلا الله تَعَالَى.
  2. توحيد الأسماء والصفات: وهو الإيمان بالأسماء والصفات لله تَعَالَى الواردة في الكتاب والسنة، من دون تمثيل، ولا تشبيه، ولا تعطيل، ولا تكييف.

ودليل أنواع التوحيد الثلاثة:

قوله تَعَالَى:

﴿رَّبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَا فَٱعۡبُدۡهُ وَٱصۡطَبِرۡ لِعِبَٰدَتِهِۦۚ هَلۡ تَعۡلَمُ لَهُۥ سَمِيّٗا﴾

[مريم: 65].