Skip to content
Orodha ya Sura /

المَسَد

المَسَد is chapter 111 of the Quran and has 5 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

5 Aya Sura Na. 111
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

تَبَّتۡ يَدَآ أَبِي لَهَبٖ وَتَبَّ

Imeangamia mikono ya Abu Lahab, na yeye pia ameangamia.

Explanation & meanings · 1
  1. Imeteketea mikono ya Abu Lahab iliyo kuwa ikiwaudhi Waislamu, na yeye mwenyewe amehiliki pia.

مَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُ مَالُهُۥ وَمَا كَسَبَ

Hayatamfaa mali yake, wala alivyo vichuma.

Explanation & meanings · 1
  1. Hayatolindwa na adhabu ya Mwenyezi Mungu mali yake aliyo kuwa nayo, wala cheo chake alicho kichuma.

سَيَصۡلَىٰ نَارٗا ذَاتَ لَهَبٖ

Atauingia Moto wenye mwako.

Explanation & meanings · 1
  1. Ataingia katika Moto unao waka, aungue.

وَٱمۡرَأَتُهُۥ حَمَّالَةَ ٱلۡحَطَبِ

Na mkewe, mchukuzi wa kuni,

Explanation & meanings · 1
  1. Na ataingia pia kwenye Moto mkewe huyo aliye kuwa akibeba masengenyo baina ya watu, kama alivyo ingia yeye (mumewe).

فِي جِيدِهَا حَبۡلٞ مِّن مَّسَدِۭ

Shingoni mwake iko kamba iliyo sokotwa.

Explanation & meanings · 1
  1. Juu ya shingo yake itakuwa kamba ya mtende ya kumtesa.