Skip to content
Orodha ya Sura /

القَارعَة

القَارعَة is chapter 101 of the Quran and has 11 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

11 Aya Sura Na. 101
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

ٱلۡقَارِعَةُ

Inayo gonga!

Explanation & meanings · 1
  1. AL-QAARIA'H, Inayo gonga, ni Kiyama, ambacho kinaanza kwa mpulizo wa mwanzo wa barugumu, na kinaishia itapo katwa hukumu baina ya watu.

مَا ٱلۡقَارِعَةُ

Nini Inayo gonga?

Explanation & meanings · 1
  1. Kitu gani kilicho cha ajabu zaidi katika ukuu wake, na khatari zake na kitisho chake!

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡقَارِعَةُ

Na nini kitacho kujuilisha nini Inayo gonga?

Explanation & meanings · 1
  1. Na kitu gani kitacho kujuulisha hali ya AL-QAARIA'H katika kitisho chake juu ya nafsi za watu?

يَوۡمَ يَكُونُ ٱلنَّاسُ كَٱلۡفَرَاشِ ٱلۡمَبۡثُوثِ

Siku ambayo watu watakuwa kama nondo walio tawanyika;

Explanation & meanings · 1
  1. Siku hiyo watu watakuwa kama vipepeo kwa wingi na kuhangaika kulia na kushoto, madhaifu na wanyonge!

وَتَكُونُ ٱلۡجِبَالُ كَٱلۡعِهۡنِ ٱلۡمَنفُوشِ

Na milima itakuwa kama sufi zilizo chambuliwa!

Explanation & meanings · 1
  1. Na milima itakuwa kama sufi iliyo tiwa rangi na kuchambuliwa kwa kutapanyika vipande mbali mbali na kupeperuka katika anga huku na huku.