Utakapo ulizwa ni ipi dhambi kubwa ambayo aliasiwa Mwenyezi Mungu kwayo?
السؤال
Swali/ Utakapo ulizwa ni ipi dhambi kubwa ambayo aliasiwa Mwenyezi Mungu kwayo?
الجواب
Jawabu/ Sema: Ni Ushirikina amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:{Hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Maryamu! Na hali Masihi mwenyewe alisema: Enyi Wana wa Israili! Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Kwani anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharamishia Pepo na mahala pake ni Motoni. Na walio dhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru} (Al-Maida 72) na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi kushirikishwa na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye} (Annisaa 48) kitendo cha kuwa Mwenyezi Mungu hasamehi dhambi za Mshirikina akifa hajatubia ni alama kuwa Shirki ni dhambi kubwa, kinacho bainisha hilo ni kauli ya Mtume rehma na amani ziwe juu yake pindi alipo ulizwa: ni ipi dhambi kubwa? akasema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (ni kumfanya Mwenyezi Mungu kuwa ana msaidizi wake au mfano wake katika viumbe ilihali yeye amekuumba...) Imepokelewa na Bukhari na Muslim.
Ushirikina: Ni Mtu kumjalia Mwenyezi Mungu kuwa na msaidizi wake ambae wako sawa katika kazi zake au anayo sifa miongoni mwa sifa zake, katika Malaika au Mtume au Walii namfano wake, anaamini kuwepo chochote kwa kiumbe huyo katika sifa za Mwenyezi Mungu na mambo yanayo Muhusu yeye ikiwemo kuumba au ufalme au kupangikia mambo yoote ya wajawake, au akajikurubisha kwake akawa anamuomba, au kumtarajia, au kumuogopa, au anategemea, au anataka kwake kinyume cha Mwenyezi Mungu au pamoja na Mwenyezi Mungu, akakifanyia chochote katika aina za ibada za mali au mwili za dhahiri au zilizo jificha.