Skip to content

Utakapo ulizwa: ni zipi aina za Unafiki?

السؤال

Swali/ Utakapo ulizwa: ni zipi aina za Unafiki?

الجواب

Jawabu/ sema: Unafiki upo aina mbili, Unafiki mkubwa na unafiki mdogo.

Unafiki mkubwa: ni kudhihirisha Uislam na kuficha ukafiri na hizi ni katika hathari zake kubwa kuuchukia uislam na kuuchukia ushindi wake na kuwachukia waislam na kufanya bidii ya kuwapiga vita na kuharibu dini yao.

Unafiki mdogo ni kujifananisha na vitendo vya wanafiki bila kuficha ukafiri, kama mfano anayesema uwongo anapoongea na anapo ahidi hatimizi na anapo aminiwa anafanya hiyana, amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake (Alama za mnafiki ni tatu, Akiongea anasema uongo, akiaminiwa anafanya hiyana na anapo ahidi hatimizi)Imepokelewa na Imamu Bukhar.