Skip to content

Utakapo ulizwa ni vitu gani vinavyo tengua Uislam?

السؤال

Swali/ Utakapo ulizwa ni vitu gani vinavyo tengua Uislam?

الجواب

Jawabu/ sema: Chenye kutengua maana yake ni chenye kubatilisha na chenye kuharibu, Wakati wowote kinapotokea kwenye jambo uharibu, kama vile vibatilisho vya udhu ambavyo mwenye kuvifanya vinambatilisha udhu na analazimika kutawadha tena, mfano wake ni mfano vinavyobatilisha uislamu, mja anapovifanya uislam wake unaharibika na kubatilika na mtendaji anatoka katika uislamu na kuwa kafiri na wana wa chuoni wametaja katika mlango wa kuritadi na hukmu za mwenye kuritadi wametaja aina nyingi za vitu ambavyo vinaweza kumfanya Muislamu akaritadi na kutoka katika dini yake ikawa halali damu yake na mali yake na vitu vyenye hatari zaidi na vikubwa na nivingi kwa kutokea na vile ambavyo wanakubaliana wana wa chuoni kuwa vinatengua, ni vitenguzi kumi navyo: 1:Kumshirikisha Allah katika Ibada amesema Allah mtukufu: (Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi kushirikishwa na kitu. Lakini Yeye husamehe yasiyo kuwa hayo kwa amtakaye. Na anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu basi huyo amepotea upotovu wa mbali.) (Annisai 116). Na amesema Allah mtukufu {Kwani anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharimishia Pepo na mahala pake ni Motoni. Walio dhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru.} (Almaida 72), miongoni mwa kumshirikisha mwenyezi Mungu katika Ibada ni kuviomba visivyo kuwa Allah na kuviomba nusra na kujikinga kwavyo na kuweka nadhiri na kuvichinjia, kama anayemchinja jini au kaburi au walii akiwa hai au hakuwa maiti kwa lengo la kuleta manufaa au kuzuia shari kama wanavyofanya wajinga wanaidanganywa kwa uongo na shubha za waganga waongo na watu wa mazingara.

2: Mwenye kujalia baina yake na baina ua Allah wasaidizi akiwaomba kupona na kumtegemea katika kupata matakwa yake na wanawategemea katika kupata mahitaji yake ya kidunia na ya akhera, mtu huyo itakuwa amekufuru kwa makubaliano ya wana wa chuoni ,amesema Allah mtukufu): (sema hakika mimi ninamuomba mola wangu na simshirikishi na chochote) (Al Jinni 20).

3. Mtu ambae hakukufurisha washirikina au akatilia shaka katika ukafiri wao, au akasahihisha madhehebu yao ya ukafiri. Amesema Allah Mtukufu: {Na Mayahudi wanasema: Uzeir ni mwana wa Mungu. Na Wakristo wanasema: Masihi ni mwana wa Mungu. Hiyo ndiyo kauli yao kwa vinywa vyao. Wanayaiga maneno ya walio kufuru kabla yao. Mwenyezi Mungu awaangamize! Wanageuzwa namna gani hawa!} (Tawba 30) kwasababu kuridhia ukafiri ni ukafiri na dini haiswihi dini ispokuwa kwa kukufuru vyote vinavyo abudiwa kinyume cha Allah.(Twaghuti) na kuitakidi ubatili wa dini zote zisizokuwa uislam na kuzichukia na kujitakasa kutokana na dini hizo na wafuasi wa hizo dini na kupigana nao kwa kadri ya uwezavyo.

  1. Mwenye kuitakidi kwamba uongofu usiokuwa wa Mtume rehma na amani ziwe juu yake, ndio ulio kamilika kuliko uongofu wake, au akaitakidi kwamba hukumu ya asiyekuwa mtume ndio nzuri kuliko hukumu yake, Kama mfano wa yule anae fadhilisha hukumu za Matwaghuti na sheria za viumbe kuwa ndio bora kuliko sheria za Allah na Mtume wake, amesema Allah Mtukufu: {La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo hitalafiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utayo toa na wanyenyekee kabisa} (Nisaai 65). Mwenye kutanguliza kauli za Mashekh wa upotevu na mambo yao ya kizushi juu ya sunnahh za Mtume zilizo sahihi akiwa anajua akiwa anajua kuwa hizo sunnahh zimethibiti kuwa ni zamtume, Mwenyekufanya hivyo atakuwa ni kafiri kwa ijimai ya wanachuoni.

5.Mwenye kuchukia chochote katika mambo aliyo kuja nayo Mtume rehma na amani ziwe juu yake, Hatakama atayafanyia kazi, akiyachukia atakuwa amekufuru, Amesema Allah mtukufu: {Hayo ni kwa sababu waliyachukia aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi akaviangusha vitendo vyao}. (Muhammad 9).

  1. Mwenye kufanya masihara na dini aliyo kuja nayo Mtume rehma na amani ziwe juu yake, kama mwenye kufanya mzaha na baadhi ya sheria zake na hukumu zake na sunnahh zake na yale aliyo yaeleza, au anafanya masihara na yale aliyo yaeleza Mtume katika malipo ya waja watakao fanya mema, au adhabu kwa wenye kufanya Maasi katika yale aliyo yaeleza Mtume rehma na amani ziwe juu yake, mwenye kufanya masihara na hayo yalio tajwa atakuwa amekufuru na ushahidi ni Kauli ya Allah Mtukufu: {(Sema: Mlikuwa mkimfanyia masihara Mwenyezi Mungu na ishara zake na Mtume wake? Msitoe udhuru; mmekwisha kufuru baada ya kuamini kwenu! Tukilisamehe kundi moja kati yenu, tutaliadhibu kundi jingine kwa kuwa wao ni wakosefu) } (Tawba 65-66)
  2. Uchawi na hauwi ila kwa kutumia majini na mashetani na kuwashirikisha na kufanya mambo ambayo ni yaukafiri, kwa sababu ya kupata radhi zao, miongoni mwa uchawi nikufanya jambo la ajabu lenye kuathiri hisia za watu mwenye kufanya mamno hayo au akaridhia atakuwa amekufuru na ushahidi ni kauli ya Allah Mtukufu: {Wala hao hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni mtihani; basi usikufuru}. ( Al Baqara 102).

8.Ni kujumuika na washirikina na kuwasaidia ili wawashinde waislam na dalili ni kauli ya Allah Mtukufu {Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu} (Al Maidah 51).

9.Mwenye kuitakidi kwamba baadhi ya waislam wanaruhusiwa kutoka katika sheria ya Muhammad rehma na amani ziwe juu yake kama Hidhri alivyo toka katika baadhi ya sheria ya nabii Musa rehma ziwe juu yake, mwenye kuitakidi hivyo atakuwa kafiri. dalili ni kauli ya Allah Mtukufu : {Na anaye tafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye akhera atakuwa katika wenye hasara}. (Al Imran 85)

10.Ni kuipuuzia dini ya Allah hajifunzi dini wala kuyafanyia kazi maamrisho yake na dalili ni kauli ya Allah Mtukufu: {Na ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye kumbushwa kwa Ishara za Mola wake Mlezi, kisha akazikataa? hakika Sisi tutajilipiza kwa wakosefu} (Sajdah 22). na maana ya kuipuuzia Dini: ni kuto kujifundisha yale yanayo paswa kuyajua katika dini katika yale ambayo ni wajibu katika dini kama kujifunza misingi ya dini kama itikadi na ibada.

Baada ya kutaja hayo ambayo yanabatilisha uislam inapendeze tukawazindua watu kuhusu mambo mawili muhimu nayo:

  1. Ni kwamba lengo la kutaja hivi vitenguzi nikutaka kuwakumbusha watu na kuwatahadharisha, hakika shetani na wasaidizi wake miongoni mwa watu wanao potosha dini na kuigeuza wanasubiri mapungufu kwa Waislamu ili watumie nafasi ya kughafilika kwao na ujinga wao ili wawatoe katika Dini ya haki na ili wawatowe katika njia ya pepo na kuwaelekeza kunako njia ya Motoni.
  2. Hivi vitenguzi vya uislam kuambatanisha na hali ya kimaisha ili kumpa hukumu kwamba huyu ni kafiri au sio kafiri ni katika majukumu ya wanachuoni wakubwa walio zama katika elimu, wao ndio wanao jua dalili na hukumu na sababu na vigezo vya kushuka hukumu mbalimbali kwa watu na sio kwa kila mtu anaweza kutoa hukumu hiyo.