Skip to content

Ukiulizwa: Je, Maneno yalio tamkwa na ulimi kwa makosa bila kukusudia, au Maneno Machafu yana adhari juu ya tawhiid? Je! mwenye kuyasema hayo yanaweza kumuondoa kunako njia ya Uislam, au ni madhambi madogo?

السؤال

Swali/ Ukiulizwa: Je, Maneno yalio tamkwa na ulimi kwa makosa bila kukusudia, au Maneno Machafu yana adhari juu ya tawhiid? Je! mwenye kuyasema hayo yanaweza kumuondoa kunako njia ya Uislam, au ni madhambi madogo?

الجواب

Jawabu/ Jambo la kutamka na ulimi ni jambo hatari sana kwa tamko moja tu mtu anaingia katika Uislam na mtu anaweza kutoka katika uislam kwa tamko moja tu na Allah atukinge na matamshi ya ulimi ambayo mtu anatamka bila kutarajia yana tofautiana miongoni mwake kuna maneno ya kikafiri ambayo yanayo batilisha Uislam na kuharibu ibada za mtu, kama vile kumtukana Mwenyezi Mungu na Mtume wake rehma na amani ziwe juu yake, au maneno ya kuwasifu watu wenye cheo na mawalii sifa za Mwenyezi Mungu na kuwaomba msaada na kunasibisha kwao mambo yote ya heri ambayo yanayopatikana kwa wanadamu na katika hayo ni kuwasifu sifa zilizo pindukia zinazo wanyanyua juu ya viumbe wengine na kuwaapia na kufanya masihara sheria ya Mwenyezi Mungu na hukumu zake, au kuchukia hukumu za Mwenyezi Mungu alizo shusha kwa waja wake, au kupinga hukumu zake alizo zipanga katika matukio yenye kuumiza katika mambo yasiyo pendeza katika mambo yanayo patikana katika dunia kama misiba katika mwili na mali na watoto na mengineyo

Miongoni mwa madhambi makubwa ambayo yanaharibu imani ya mtu na kuiharibu ni kusengenya na Kuteta tunatakiwa tuyatahadhari ukweli wa kutahadhari, tuhifadhi ndimi zetu kutokana na kila tamko ambalo linalo pingana na sheria ya Allah na sunnahh za Mtume wake rehma na amani ziwe juu yake, amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Hakika mja anaweza kutamka neno moja linalo mridhisha Allah bila kulichukulia manani, ila Mwenyezi Mungu anamyanyua daraja kubwa na hakika mja anaweza kutamka neno katika maneno yanayo mchukiza Mwenyezi Mungu bila kulichukulia manani anamzamisha kwa sababu ya neno hilo katika Moto wa Jahanam). Imepokelewa na Imamu Bukhari.