Utakapo ulizwa: ni zipi aina za Ukafiri?
السؤال
Swali/ Utakapo ulizwa: ni zipi aina za Ukafiri?
الجواب
Jawabu/ Sema: Ukafiri upo aina mbili:
1.Ukafiri mkubwa: unamtoa mtu katika uislam nao ni wenye kupingana na uislam kama mwenye kumtukana Allah au mtume wake au dini yake au akafanya masihara au istihzai katika sheria ya uislam au akaikataa habari ya Allah au amri yake au makatazo yake, akakadhibisha yale aliyoyaeleza Allah na mtume wake au akakanusha chochote alicho kifaradhisha Allah kwa waja wake, Au akahalalisha aliyoharamisha Allah na mtume wake. Amesema Allah mtukufu: (Sema: Mlikuwa mkimfanyia masihara Mwenyezi Mungu na ishara zake na Mtume wake? (65) Msitoe udhuru; mmekwisha kufuru baada ya kuamini kwenu! Tukilisamehe kundi moja kati yenu, tutaliadhibu kundi jingine kwa kuwa wao ni wakosefu) (Tauba 65-66.)
2.Ukafiri mdogo nao ni ule ambao dalili za kisheria zimeuita ni ukafiri na sio ukafiri mkubwa kwa jina jingine unaitwa kukufuru neema au ukafiri mdogo, kama vile muislamu kupigana na muislamu mwenzake, kujivua unasabu na kuomboleza na mfano wake katika mambo ya kijinga amesema mtume rehma na amani ziwe juu yake (kumtukana muislamu ni uovu na kupigana naye ni ukafiri) Imepokelewa na Bukhar, amesema mtume rehma na amani ziwe juu yake: (watu wa aina mbili katika watu wana ukafiri: mwenye kutia dosari kwa nasabu na kuomboleza kwa maiti), imepokelewa na Muslim: Ibada hizi hazimtoi mtu katika Uislam lakini ni katika madhambi makubwa Allah atuepushe.