Utakapo ulizwa ni vingapi vigawanyo vya Ushirikina?
السؤال
Swali/ Utakapo ulizwa ni vingapi vigawanyo vya Ushirikina?
الجواب
Jawabu/ Sema: Ushirikina umegawanyika mara mbili:
1.Shirki Kubwa: Nayo ni kukifanyia ibada kisichokuwa Mwenyezi Mungu, Kama kutegemea kwa asiekuwa Mwenyezi Mungu, au kuomba msaada kwa walio kufa, au kukichinjia kisichokuwa Mwenyezi Mungu, au kutoa nadhiri kwa kisichokuwa Mwenyezi Mungu, au kukisujudia kisichokuwa Mwenyezi Mungu, au kuomba nusra kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu katika mambo ambayo hakuna mwenye uwezo nayo ila ni Mwenyezi Mungu, kama kuomba nusra kwa wasio kuwepo, au walio kufa na hakuna anaefanya mambo haya ya kijinga ila mwenye kuitakidi uwezo wao wa kujibu na kwamba wana uwezo wa kufanya mambo ambayo hakuna mja anaweza kufanya ila ni Mwwnyezi Mungu, anakuwa kwa kitendo hicho ameitakidi kwa kiumbe huyo kuwa na mambo yanayo muhusu Mwenyezi Mungu, anakinyenyekea na kujidhalilisha kwake udhalili wa kukiabudu na anakitegemea katika mambo yake na anaomba nusra kwa kitu hicho na anakiita akiomba mambo ambayo hakuna kiumbe anaeweza kumtimizia. Na jambo la ajabu ni mtu kuomba nusra kwa kitu ambacho hakina uwezo wowote hakimiliki kujiletea manufaa wala kujikinga na Madhara, hakimiliki kifo wala uhai wala kufufuliwa na mtu ambae hawezi kujiletea manufaa wala kuzuia madhara juu ya nafsi yake vipi atamiliki vitu hivyo kwa watu wengine, kitendo hiki ni kama mfano wa mtu anae zama baharini kumuomba msaada mwenzake ambae anazama.Utakasifu ni wa Mwenyezi Mungu! Vipi yamefunga macho ya washirikina na kuondoka kwa akili zao wakadiriki kufanya Ushirikina unaopingana na sheria ya Mwenyezi Mungu, Ushirikina unao pingana na akili salama, pia Ushirikina unao pingana na Maumbile!
2.Shirki ndogo: Mfano wa kujionyesha kama alivyo sema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Jambo kubwa ambalo ninalo chelea kwenu ni Shirki ndogo, akaulizwa kuhusu shirki ndogo akasema: Kujionyesha (Riyaa) Imepokelewa na Muslim na mfano mwingine wa shirki ndogo ni kuapia kwa kisichokuwa Mwenyezi Mungu, amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Mwenyekuapia kisichokuwa Mwenyezi Mungu atakuwa amekufuru au amefanya shirki) Imepokelewa na Tirmidhy.