Chuja matokeo
Kadi 335
الموضوعات
الموضوعات (13)
التصنيف الشرعي
Filter ▾
حجم المحتوى3
Jawabu/ Sema: Ndio, amesema Mwenyezi Mungu mtukufu: {Wanaonyeshwa Moto asubuhi na jioni. Na itapo fika Saa ya Qiyama patasemwa: Waingizeni watu wa Firauni katika adhabu kali kabisa!} (Ghafir 46) na amesema Mwenyezi Mungu: {Na laiti ungeli ona Malaika wanapo wafisha wale walio kufuru wakiwapiga nyuso zao na migongo yao na kuwaambia: Ionjeni adhabu ya Moto!} (Anfal 50) na kauli ya Mwenyezi Mungu: {Mwenyezi Mungu huwatia imara wenye kuamini kwa kauli ya imara katika maisha ya dunia na katika akhera} (Ibrahim 27) na imekuja katika hadithi Qudsiy ndefu kutoka kwa swahaba Baraa -radhi za Allah ziwe juu yake-: (Atanadi mwenye kunadi mbinguni akisema: Amesema ukweli mjawangu mtandikieni peponi na mumvishe mavazi ya watu wa peponi na mfungulieni mlango wa pepo, inatoka katika pepo hiyo harufu nzuri kisha kaburi lake linapanuliwa, inakuwa kubwa kiasi cha upeo wa macho yake na hakika kafiri, kisha akataja hali anayo ipata wakati wa kufa kwake, akasema: Kisha roho yake inarejeshwa katika mwili wake, kisha wanamjia malaika wawili, kisha wanamkalisha, kisha wanamuuliza: Nani mola wako? atajibu: haa haa sijuwi, kisha wanamuuliza ni ipi dini yako? atajibu haa haa sijuwi, kisha watamuuliza niyupi huyo mwanaume alie tumwa kwenu? atajibu: haa haa sijuwi, atanadi mwenye kunadi mbinguni akisema: huyo amesema uwongo mtandikieni matandiko ya motoni na mvisheni mavazi ya watu wa motoni na mfungulieni mlango wa moto, kisha ule moto na joto na sumu zake vinamjia, kisha kaburi linambana mpaka mbavu zake zinatofautiana. Amezidisha mpokezi katika riwaya: (Kisha analetewa malaika asie ona wala hazungumzi, akiwa na nyundo kubwa na nzito ya chuma, laiti ungepigwa mlima kwa nyundo hiyo mlima ungesagika ukawa kama mchanga, kisha anapigwa nayo pigo moja ambalo viumbe vyote vya mashariki na magharibi vinasikia ila watu na majini hawasikii). Imepokelewa na Abudaud. Kwa sababu ya jambo hili ndio maana Mtume akatuamrisha tujilinde kwake na adhabu za kaburini katika kila swala.
Jawabu/ Sema: ndio watamuona mola wao siku ya Akhera na miongoni mwa dalili juu ya hilo ni kauli ya Mwenyezi Mungu mtukufu: {Nyuso za watu siku ya qiyama zitakuwa na nuru (22) zikimuangalia mola wao mlezi} alqiyama (22-23) na kauli ya Mtume rehma na amani ziwe juu yake, (Hakika nyinyi mtamuona mola wenu) imetolewa na Imamu Bukhari na Muslim, na zimekuja hadithi zilizo sahihi kutoka kwa Mtume rehma na amani ziwe juu yake katika kuthibitisha kuwa waumini watamuona Mola wao Mtukufu na maswahaba wa Mtume rehma na amani ziwe juu yake wamekubaliana juu ya hilo na Mataabii na walio wafuata kwa wema. Atakae kanusha kuonekana kwa Mwenyezi Mungu atakuwa amemfanyia uadui Mwenyezi Mungu na Mtume wake rehma na amani ziwe juu yake na atakuwa amekhalifu njia ya waislam kuanzia maswahaba wa Mtume rehma na amani ziwe juu yake na walio wafuata kwa wema. Ama Mwenyezi Mungu kuonekana Duniani haiwezekani kuonekana kwa kauli ya Mtume rehma na amani ziwe juu yake: ( Hakika nyinyi hamta muona mola wenu mpaka mtakapo kufa) na nabii Mussa -amani ziwe juu yake-zama alipo muomba Mwenyezi Mungu amuone duniani kama ilivyo kuja katika kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na alipokuja Musa kwa wakati uliowekwa na Akasema na yeye Mola, alisema Musa Mola wangu naomba nikuone, akamjibu Mwenyezi Mungu Akamwambia, Hutoniona} (Al-Aaraf 143).
Jawabu/ Sema: Inakuwa kwa yakini ya mkato kwamba kila kitu kinakuwa kwa hukumu ya Mwenyezi Mungu na mipangilio yake, hakiwi kitu chochote ila kwa utashi wake, yeye ndie alie umba vitendo vya waja wake vya heri na shari, na akawaumba waja wake katika maumbile ya heri na ya kukubali haki, na akawapa akili yenye kupambanua na akawaruzuku utashi ambao watachagua wanacho kipenda kwa utashi huo, na akawabainishia haki na akawatahadhalisha na batili, akamuongoza anae mtaka kwa fadhila zake na akampoteza anae mtaka kwa uadilifu wake, yeye ndie mwenye hekima na ni mjuzi mwenye huruma, haulizwi kwa anacho kifanya na waja wanaulizwa kwa kila wanacho kifanya.
Daraja za Qadar ni nne:
Daraja ya kwanza: Ni kuamini elimu ya Mwenyezi Mungu kwamba yeye amekizunguka kila kitu, yeye ni mjuzi kwa yale yalio tokea na yale yanayo tokea na yale ambayo hayajatokea, kama yangetokea yangekua vipi.
Daraja la pili: Ni kuamini kwamba Mwenyezi Mungu aliandika kila kitu.
Daraja la tatu: Ni kuamini kwamba kwa Mwenyezi Mungu hakiwi chochote ila kwa utashi wake.
Daraja la nne: Ni kuamini kwamba Mwenyezi Mungu ndie alie umba kila kitu, yeye ndie alie umba dhati ya vitu na matendo na maneno na harakati na utulivu na sifa na kila kitu katika ulimwengu wa juu na wachini na wa aridhini, na dalili za yalio tangulia ziku nyingi katika kitabu cha Mwenyezi Mungu na suna za Mtume.
Jawabu/ Sema: Haisemwi kuwa Mwanadamu anaendeshwa katika mambo yote au amekhiyarishwa yote mawili ni makosa, dalili za kitabu na sunnahh zimeonyesha kuwa mwanadamu ana utashi wake na kwamba yeye ndie mtendaji kwa uhakika wake, lakini yote hayo hayatoki katika elimu ya Mwenyezi Mungu utashi wake, kinacho bainisha hayo ni kauli ya mwenyezi Mungu: {Kwa mwenyekutaka miongoni mwenu, kulingana na kushikamana juu ya haki na Imani(28) Wala nyinyi hamtotaka isipokuwa kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe wote} (Takwiir 28-29) na amesema Mwenyezi Mungu: {Mwenye kutaka ataizingatia(55) na hawata zingatia na kuwaidhika ila akitaka Mwenyezi Mungu yeye ndie anae stahiki kuogopwa na yeye ndie anaestahiki kusamehe} (Mudathir 55-56)
Jawabu/ sema: Haiswihi imani bila matendo bali matendo ni lazima kwasababu matendo ni nguzo katika imani, ilivyo tamkwa na wanachuoni nikwamba ninguzo katika Imani, na wanachuoni wamekubaliana katika hilo kwamba imani ni kauli na vitendo na ushahidi juu ya hilo ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {na atakae kuendea MwenyeziMungu akiwa amefanya matendo mema hao ndio wenye daraja la juu} tah 75, Mwenyezi Mungu akaweka sharti la imani na matendo pamoja ili mtu aingie peponi.
Jawabu/ Sema: ni Tano, nazo: Ni kushahidilia kuwa hapana mungu apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mungu mmoja na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na kusimamisha swala na kufunga ramadhani na kutoa zaka nakuhiji katika nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu.
Amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Uislam umejengewa juu ya mambo matano: Ni kushahidilia kuwa hapana mungu apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mungu mmoja na kwamba muhammad ni mtume wa Mwenyezi Mungu na kusimamisha swala na kutoa zaka na kuhiji katika nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu na kufunga Ramadhani) Imepokelewa na Bukhari na Muslim.
Jawabu/ sema: Shahada kuwa hapana Mungu apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu: Maana yake: Hakuna wa kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu kama ilivyo katika kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na pale Ibrahim alipo mwambia baba yake na kaumu yake: Hakika mimi ninajitenga mbali na hayo mnayo yaabudu. (26) Isipo kuwa yule aliye niumba, kwani Yeye ataniongoa.(27) Na akalifanya hili liwe neno lenye kubaki katika vizazi vyake ili warejee}.(Zukhruf26-28) na amesema Mwenyezi Mungu:{ Kwani huoni kwamba Mwenyezi Mungu huuingiza usiku katika mchana na huuingiza mchana katika usiku na amedhalilisha jua na mwezi? Vyote hivyo vinakwenda mpaka wakati ulio wekwa. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayo yatenda}. (Luqman 29)
Na maana ya Shahada ya kuwa muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu: Ni kuyakinisha yakwamba ni mja wa Mwenyezi Mungu na nimtume wake na kwamba yeye ni mtumwa haabudiwi na ni mtume hakadhibishwi, anatiiwa kwa yale aliyo yaamrisha na anasadikishwa kwa yale aliyo yaeleza na yanatengwa mbali yale yote aliyo yakataza na kuyakemeya na asiabudiwe Mwenyezi Mungu ila kwa sheria yake bila kuzidisha wala kupunguza.
Na haki ya Mtume rehma na amani ziwe juu yake juu ya Ummah wake, ni kumuheshimu na kumtukuza na kumpenda na kumfuata, katika kila wakati na zama kwa kadri ya uwezo, amesema Mwenyezi Mungu: {Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu.} (Al Imran 31)
Jawabu/ Sema: Neno la tawhiid halitoshi kutamkwa bila ya kuitakidi na kuzingatia na kusimamia mambo yanayo pelekea kutamka neno hilo na kujiepusha na mambo yanayo yatengua, bali neno hilo lina masharti saba, wanachuoni wameyatoa masharti hayo katika dalili ya kisheria, wakaziandika na kuzitolea dalili katika Qur'an na Sunnah nazo:
1- Elimu kwa maana yake katika kukanusha na kuthibitisha, ni kujua kuwa hakika Mwenyezi Mungu hana mshirika na yeye ndie anaestahiki kuabudiwa na dalili ambazo zimeonyesha kukanusha Uungu kwa asiekuwa Mwenyezi Mungu na kujua mambo ya lazima na yanayo takiwa kufanywa baada ya kutamka neno hilo pia nakujua mambo yanayo batilisha neno hilo, amesema Mwenyezi Mungu mtukufu: {Basi jua ya kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu} (muhammad 19) na amesema Mwenyezi Mungu: { isipo kuwa anaye shuhudia kwa haki na wao wanajua} (Zukhruf 86), amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: Atakae kufa akiwa anajua kuwa hakuna Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Allah ataingia peponi) Imepokelewa na Imamu muslim.
2- Yakini nayo: nikuitakidi kwa mkato juu ya neno hilo la shahada, yakini ambayo inayo pingana na Shaka au wasiwasi, yakini ilio thibiti katika moyo, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: { Hakika Waumini ni wale walio muamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake tena wasitie shaka kabisa na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao. Hao ndio wakweli}(Al-Hujrat 15) na amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Atakae sema ninashahidilia kuwa hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu na mimi ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu mja hakutani na Mwenyezi Mungu akiwa na shahada hizo mbili bila ya kuwa na mashaka katika hizo shahada ila ataingia peponi) Imepokelewa na Muslim.
3.Ikhlasi inayo pinga Ushirikina, kwasababu ya kusafisha Ibada na kuitakatisha kutokana na uchafu wa ushirikina, au kujionyesha. Amesema Allah mtukufu: {Hakika dini Safi ni ya Mwenyezi Mungu tu.} ( Zumar 3) na amesema Allah mtukufu: {Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia dini} (Albayyinah 5) na amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: ( Watu watakao pata mafanikio ya uombezi wangu siku ya Qiyama, ni mtu aliesema Lailaha ila Allah akiwa na Ikhlas katika moyo wake na nafsi yake) Imepokelewa na Imamu Bukhary.
4. Mapenzi (Mahaba) ya neno hilo la tawhiid na yale ambayo yanayo elezwa na neno hilo, na kufurahia hilo, na kuwapenda wenye kulisema neno hilo, na kukithirisha mapenzi kwao, na kuwachukia wanao lipinga neno hilo na kujitenga mbali nao wakiwemo makafiri, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:,{Na katika watu wapo wanao chukua waungu wasio kuwa Mwenyezi Mungu. Wanawapenda kama kumpenda Mwenyezi Mungu. Lakini walio amini wanampenda Mwenyezi Mungu zaidi sana} (Albaqara 165) na amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Mambo matatu atakae kuwa nayo atapata utamu wa imani, awe Allah na Mtume wake ndio vipenzi vyake kuliko vitu vyote, na ampende mtu hampendi kwa lolote ila ni kwa ajili ya Allah, na achukie kurudi katika ukafiri kama anavyo chukia kutupwa Motoni) Imepokelewa na Imamu Muslim.
5. Ukweli unao pingana na Uwongo na ukweli unakuwa kwa Moyo kuafikiana na viungo katika kile kilicho tamkwa na ulimi ambacho ni neno la Tawhiid, viungo vinasadikisha moyo kwa maneno yaliyo semwa na moyo huo vinafanya Ibada za wazi na za ndani, Amesema Allah mtukufu:{Mwenyezi Mungu atawatambulisha walio wa kweli na atawatambulisha walio waongo} (Al-Ankabuti 3) na amesema Allah Mtukufu: {Na aliye ileta Kweli na akaithibitisha - hao ndio wachamngu} (Azzumar 33) na amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Atakae kufa akiwa anashahidilia kuwa Hapana Mungu apasae kuabudiwa kwa haki na Muhammad ni mtume wa Allah akiwa ni mkweli katika moyo wake ataingia peponi) Imepokelewa na Imamu Ahmad.
6. Kuzingatia, kwa kunyenyekea kwa ajili ya Allah kwa kumpwekesha katika ibada na kuleta haki zake kwa kutekeleza maamrisho yake nakujiepusha na makatazo yake kwa Ikhlasi kutaka thawabu na kutarajia malipo kwa Allah na kwa kumuogopa Allah, Amesema Allah mtukufu: {Na rejeeni kwa Mola wenu Mlezi na silimuni kwake} (Zumar 54) na amesema Allah Mtukufu {Na mwenye kuuelekeza uso wake kwa Mwenyezi Mungu naye akawa anafanya wema, basi huyo hakika amekwisha kamata fundo lilio madhubuti} (Luqman 22)
- Kukubali kunako pingana na kukataa na inakuwa kwa moyo kukubali neno la tawhiid na yale yanayo patikana katika tamko hilo, lakini neno hilo halipokelewi kwa mwenye kujidai kufuata neno hilo kwa kujibaguwa na wengine au kwa kiburi, Anasema Allah mtukufu: { Wao walipo kuwa wakiambiwa La ilaha illa 'Llahu Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu tu, wakijivuna} (Swafati 35). Huyo hawi muislam
Jawabu/ Sema: Ni muhammad Bin Abillah Bin AbdilMutwalib Bin Hashim Bin Abdilmanafi. Mwenyezi Mungu alimchagua kutoka katika kabila la kiqurayshi nao ni Watoto wa Ismaili Bin Ibrahim Amani ziwe juu yao, Mwenyezi Mungu alimtuma kwa majini na watu na akamshushia kitabu na hekima na akamfanya ni mtume bora na ni mbora wa Mitume rehma na amani ziwe juu yake.
Jawabu/ Sema: Ibada ya kwanza aliyo ifaradhisha ni Imani ya kumuamini yeye Mwenzi Mungu Mtukufu na kukufuru vyote visivyokuwa yeye (Twaghuti), kama alivyo sema: {Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu na muepukeni Shetani. Basi kati yao wapo alio waongoa MwenyeziMungu. Na kati yao wapo ambao ulio wathibitikia upotovu. Basi tembeeni katika ardhi, muangalie ulikuwaje mwisho wa wanao kanusha} ( Annahli 36) Na Twaghuti: Ni kila jambo ambalo mja amechupa mipaka katika katika kinacho fuatwa au kuabudiwa au kutiiwa.
Jawabu/ Sema: Amebainisha Allah ukweli wa kubainisha malengo hayo, kwamba aliumba viumbe watu na majini ili wamuabudu yeye peke yake hana mshirika na ibada hiyo ni kutii amri zake na nikujiepkusha na makatazo yake, Amesema Allah Mtukufu: {Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi} (Adh- dhariyat 56) na amesema Allah Mtukufu: {Muabuduni Mwenyezi Mungu na msimshirikishe na chochote} (Annisaai36)
Jawabu/ Sema: Hakika Dua ni katika aina kubwa ya ibada, kama alivyo sema Allah mtukufu: {Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni. Kwa hakika wale ambao wanajivuna na kuniabudu Mimi wataingia Jahannamu wadhalilike} (Ghafir 60) na katika hadithi: Amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Dua ndio Ibada) Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy na kwa ukubwa wa dua na umuhimu wake katika dini imekuja dua katika zaidi ya aya mia tatu (300) katika Qur'an Tukufu na dua ina aina mbili:dua ya ibada na dua ya Maombi na kila kimoja hakitimii mpaka kiwe na mwenzake.
Dua ya ibada: Ni kujikurubisha kwa Allah mtukufu kwa ajili ya kupata unacho kitafuta, au kuzuia mabaya, au kuondoa madhara kwa kufanya ikhlas katika ibada za Allah mtukufu. Anasema Allah Mtukufu: {Na Dhun-Nun alipoondoka hali ameghadhibika na akadhani ya kwamba hatutakuwa na uwezo juu yake. Basi aliita katika giza: Hapana mungu isipo kuwa Wewe Subhanaka Uliye takasika. Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu (87) Basi tukamwitikia na tukamwokoa kutokana na dhiki. Na hivyo ndivyo tunavyo waokoa Waumini} (Al-Anbiyaa 87-88).
Dua ya Maombi: ni kuomba mambo yenye manufaa kwa muombaji miongoni mwa kuleta manufaa, au kuondoa madhara. Amesema Allah Mtukufu: {Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tumeamini, basi tufutie madhambi yetu na tuepushe na adhabu ya Moto} (Al-Imran 16)
Dua kwa aina zake mbili ndio ubongo wa ibada kwa uchache wake nayo ni ibada nyepesi kwa kuiomba na ndiyo yenye cheo cha juu na athari kubwa, dua ni sababu yenye nguvu katika kuzuia mambo mabaya na mtu kupata kile anacho kitafuta kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Jawabu/ Sema: Ibada haikubaliwi kwa Allah mpaka itimize masharti mawili: Sharti la kwanza: Ibada iwe kwa ajili ya Allah mtukufu na ushahidi ni Kauli yake Mwenyezi Mungu: {Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia dini} (Albayyinah 5) na amesema Mwenyezi Mungu mtukufu: {Mwenye kutaraji kukutana na Mola wake Mlezi basi naatende vitendo vyema, wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake Mlezi} (Kahfi 110)
Sharti la pili: Iwe ibada ni yenye kuafikiana na sheria aliyo kujanayo Mtume rehma na amani ziwe juu yake na dalili ni kauli ya Mwenyezi Mungu mtukufu: {Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu} (Al-Imran31). na kauli ya Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Mwenyekufanya ibada ambayo haipo katika dini yetu basi atarudishia mwenyewe) Imepokelewa na Imamu Muslim. na kama ibada haikubaliani na uongofu wa Mtume rehma na amani ziwe juu yake hakika ibada hiyo haikubaliwi hatakama alie ifanya ameifanya kwa ajili ya Allah.
Jawabu/ Sema: Hapana, lazima vikusanyike na Nia safi ambayo ni kufanya Ibada kwa ajili ya Allah na yenye kuafikiana na sheria ya Mtume wa Allah rehma na amani ziwe juu yake. Dalili ya hayo ni Kauli ya Mwenyezi Mungu mtukufu: {Mwenye kutaraji kukutana na Mola wake Mlezi basi na atende vitendo vyema, wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake Mlezi} (Kahfi 110). Mwenyezi Mungu mtukufu akaweka sharti katika aya hii kwamba ili matendo yawe mema lazima iwe kuna nia njema na yawe matendo yako ni mema na yenye kukubaliana na sheria ya Mtume rehma na amani za Allah ziwe juu yake.
Jawabu/ Sema: Tawhiidi ina vigawanyo vitatu: 1. Tawhiid Rububiyyah: nayo ni kuitakidi kwa mkato kwamba Mwenyezi Mungu ndie muumbaji anae toa rizki na mwenye kupangikia mambo ya waja wake wote, hana Mshirika wala msaidizi na yo ni kumkwekesa Mwenyezi Mungu kwa vitendo vyake Allah, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:{Ati yupo muumba mwengine asiye kuwa Mwenyezi Mungu anaye kupeni riziki kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Hapana mungu ila Yeye tu. Basi wapi mnako geuzwa?} (Fatwir 3) na anasema Mwenyezi Mungu: {Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti}. (adh-adhariyat 58) na anasema Mwenyezi Mungu: {Anapitisha mambo yote yalio baina mbingu na ardhi} (Asajidah 5) na amesema Mwenyezi Mungu: {Fahamuni! Kuumba na amri ni zake. Ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.} (Al-Aaraf 54).
- Tawhiidul Asmaai wa swifati: nayo ni kuitakidi kwamba Mwenyezi Mungu ana majina mazuri na sifa zilizo kamilika zilizo thibiti katika Qur'an na sunnahh, bila kufananisha wala kulinganisha, wala kupindisha wala kugeuza na kwamba Mwenyezi Mungu hana mfano wa kitu chochote, amesema Mwenyezi Mungu mtukufu: { Hana mfano wa chochote na yeye nimsikivu na anaona} ( Shura 11). na amesema Mwenyezi Mungu: {Mwenyezi Mungu ana majina mazuri muombeni kupitia majina hayo}.
3. Tawhiid Al-Uluhiyyah: nayo ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu pekeyake hana mshirika katika ibada, yaani kumpwekwsha Mwenyezi Mungu katika vitendo vya waja wake inaitwa tawhiidi ya kiibada, amesema Mwenyezi Mungu: {Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia dini} (Albayyinah5) na amesema Mwenyezi Mungu:{ Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote ila tulimfunulia ya kwamba hapana mungu isipo kuwa Mimi. Basi niabuduni Mimi tu} (Al-Anbiyaai 25) na mgawanyo huu ni kwajili ya kuweka wazi maswala ya kielimu na kama sio hivyo huo mgawanyo unalazima kuwepo katika itikadi ya kila Muislam mwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu na mwnye kufuata Kitabu na sunnahh.