Skip to content

Ikiwa mwanamke anaona damu siku moja akiwa katika mzunguko wake, na siku inayofuata haoni damu mchana kutwa, ni kipi juu yake anatakiwa kufanya?

السؤال

Swali la 1:

Ikiwa mwanamke anaona damu siku moja akiwa katika mzunguko wake, na siku inayofuata haoni damu mchana kutwa, ni kipi juu yake anatakiwa kufanya?

س15: إذا رأت المرأة في زمن عادتها يومًا دمًا، والذي يليه لا ترى الدم طيلة النهار، فماذا عليها أن تفعل؟

الجواب

Jawabu la 1:

Linalo onekana ni kwamba, hii twahara au ukavu (katika sehemu za siri) uliopatikana wakati wa siku zake za hedhi, utafuata (hukumu za) hedhi, hautohesabika kama ni twahara, pamoja na hilo ataendelea kujizuia kwa yale anayojizuia kwayo mwanamke aliye katika hedhi.

Na wamesema baadhi ya wanachuoni: Mwanamke mwenye kuona damu siku moja, na siku nyingine akaona yuko twahara, basi ile damu (aliyoiona) ni hedhi, na ule usafi (aliouona) ni twahara mpaka zifike siku kumi na tano.

Na ikifika siku ya kumi na tano, inakuwa damu itokayo baada ya hapo ni damu ya ugonjwa (Istihadhwa). Na hili ndilo limetajwa kuwa ni sahihi na wanachuoni wengi katika madhehebu ya Imam Ahmad ibn Hanbali (Allah amrehemu).

ﺟ15: الظاهر أن هذا الطّهر أو اليبوسة التي حصلت لها في أيام حيضها تابعٌ للحيض، فلا يعتبر طهرًا، وعلى هذا فتبقى ممتنعةً ممّا تمتنع منه الحائض.

وقال بعض أهل العلم: من كانت ترى يومًا دمًا، ويومًا نقاءً، فالدم حيضٌ، والنقاء طهرٌ حتى يصل إلى خمسة عشر يومًا،

فإذا وصل إلى خمسة عشر يومًا صار ما بعده دم استحاضةٍ. وهذا هو المشهور من مذهب الإمام أحمد بن حنبلٍ رحمه الله.