Skip to content

Atakayeamka miongoni mwenu akiwa na afya njema katika mwili wake, akiwa na amani katika mji wake, na anamiliki chakula cha siku yake hiyo, basi atakuwa ni kama kakusanyiwa dunia (yote)

Kutoka kwa Ubaidillaah bin Mihswan Al-Answari radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:

"Atakayeamka miongoni mwenu akiwa na afya njema katika mwili wake, akiwa na amani katika mji wake, na anamiliki chakula cha siku yake hiyo, basi atakuwa ni kama kakusanyiwa dunia (yote)".

«مَنْ أَصْبَحَ مِنْكُمْ مُعَافى فِي جَسَدِهِ، آمِنًا فِي سِرْبِهِ، عِنْدَهُ قُوتُ يَوْمِهِ، فَكَأَنَّمَا حِيزَتْ لَهُ الدُّنْيَا».

Imepokelewa na Tirmidhi na bin Majah
Ni nzuri (Hasan)
Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba atakayeamka miongoni mwenu enyi waislamu akiwa mzima wa afya katika mwili wake akiwa amesalimika na matatizo na magonjwa, akiwa na amani ndani ya nafsi yake na watu wake na familia yake na barabara zake, na akiwa hana hofu, na akiwa na chakula cha halali cha kumtosha kwa siku yake; basi ni kana kwamba kakabidhiwa dunia yote nzima.

Katika Faida za Hadithi

Kumebainishwa haja ya mtu kuwa na afya na amani na nguvu.

Ni wajibu kwa mja amhimidi Mwenyezi Mungu Mtukufu na amshukuru kwa neema hizi.

Himizo la kuridhika na kuipa nyongo dunia.

Rejea

Sunanu Tirmidhiy (4/ 167) (2346).

Sunanu Ibn Maajah (5/ 253) (4141).

Zaidi (4)

بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين.

لسليم الهلالي (1/ 570).

التنوير شرح الجامع الصغير.

لمحمد الصنعاني (10/ 110).