Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 7 kati ya 839

Ondoa vichujio
Hakuacha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakati wa kifo chake Dirham moja wala Dinari, wala mtumwa wala kijakazi wala chochote, isipokuwa nyumbu wake mweupe, na silaha yake, na kipande cha Ardhi alichokitoa kama sadaka.
Sahihi Imepokelewa na Al-Bukhaariy
"Atakayeamka miongoni mwenu akiwa na afya njema katika mwili wake, akiwa na amani katika mji wake, na anamiliki chakula cha siku yake hiyo, basi atakuwa ni kama kakusanyiwa dunia (yote)".
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Tirmidhi na bin Majah
Hawakuwahi kushiba katika chakula cha ngano watu wa famili ya Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake tangu alipofika Madina, kwa siku tatu mfululizo, mpaka alipofariki.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Ilipoteremka: "Kisha hakika bila shaka mtakuja kuulizwa kuhusu neema" [Takathur: 8], akasema Zubairi: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni neema zipi tutakazooulizwa juu yake, au ni hivi vyeusi viwili tende na maji (Vyakula na vinywaji kwa ujumla)? Akasema: "Hakika bila shaka zitakuwa hizo".
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Tirmidhi na bin Majah
"Ipe nyongo dunia Allah atakupenda ,na usivitolee macho vitu vya watu, watu watakupenda".
Amesema Imamu Nawawi: Hadithi hii ni hasan Imepokelewa na Ibn Majah na wengineo kwa sanadi nzuri.
"Dunia ni Gereza la Muumini na ni Pepo ya Kafiri".
Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim
Hakuwahi kula Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake milo miwili kwa siku isipokuwa mlo mmoja utakuwa ni tende.
Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake