Skip to content
Orodha ya Sura /

التِّين

التِّين is chapter 95 of the Quran and has 8 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

8 Aya Sura Na. 95
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَٱلتِّينِ وَٱلزَّيۡتُونِ

Naapa kwa tini na zaituni!

Explanation & meanings · 1
  1. Naapa kwa tini na zaituni, kwa baraka zao na ubora wa manufaa yao.

وَطُورِ سِينِينَ

Na kwa Mlima wa Sinai!

Explanation & meanings · 1
  1. Na kwa mlima ambao juu yake ndio Mwenyezi Mungu alimsemeza Musa.

وَهَٰذَا ٱلۡبَلَدِ ٱلۡأَمِينِ

Na kwa mji huu wenye amani!

Explanation & meanings · 1
  1. Na kwa huu mji mtukufu wa Makka, ambao anaushuhudia utukufu wake mwenye kwenda uzuru, na anapata amani mwenye kuuingia.

لَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ فِيٓ أَحۡسَنِ تَقۡوِيمٖ

Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa.

Explanation & meanings · 1
  1. Kwa hakika bila ya shaka yoyote Sisi tumemuumba mtu amesimama sawa kwa umbo bora kabisa lilio nyooka, na akasifika kwa sifa nzuri kabisa.

ثُمَّ رَدَدۡنَٰهُ أَسۡفَلَ سَٰفِلِينَ

Kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini!

Explanation & meanings · 1
  1. Kisha tukamteremsha cheo mpaka akawa ni wa chini kabisa katika hao walioko chini, kwa kuacha kufanya waajibu wa hayo tuliyo muumbia.