Skip to content
Orodha ya Sura /

الشَّرح

الشَّرح is chapter 94 of the Quran and has 8 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

8 Aya Sura Na. 94
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

أَلَمۡ نَشۡرَحۡ لَكَ صَدۡرَكَ

Hatukukunjulia kifua chako?

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika tumekukunjulia kifua chako kwa kuwa tulitia ndani yake Uwongofu na Imani.

وَوَضَعۡنَا عَنكَ وِزۡرَكَ

Na tukakuondolea mzigo wako!

Explanation & meanings · 1
  1. Na tumekupunguzia mizigo iliyo kuwa mizito juu ya mgongo wako, kwa kukuunga mkono na kukusahilishia mambo yako,

ٱلَّذِيٓ أَنقَضَ ظَهۡرَكَ

Ulio vunja mgongo wako?

Explanation & meanings · 1
  1. Ambayo yalikuwa ni mazito juu ya mgongo wako.

وَرَفَعۡنَا لَكَ ذِكۡرَكَ

Na tukakunyanyulia utajo wako?

Explanation & meanings · 1
  1. Na tumelitukuza jina lako, tukalifanya linatajwa na ulimi wa kila Muumini pamoja na jina letu.

فَإِنَّ مَعَ ٱلۡعُسۡرِ يُسۡرًا

Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi!

Explanation & meanings · 1
  1. Hizo ni baadhi ya neema zetu juu yako. Basi kuwa na yakini na uweza wa Mwenyezi Mtukufu, kwani pamoja na uzito upo wepesi mwingi unao kuja nao.