ٱقۡرَأۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلَّذِي خَلَقَ
Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba!
- Ewe Muhammad! Soma unayo funuliwa kwa kufunguliwa kwa Jina la Mola wako Mlezi ambaye ni Yeye tu peke yake ndiye Mwenye uweza wa kuumba.
العَلَق is chapter 96 of the Quran and has 19 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.
ٱقۡرَأۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلَّذِي خَلَقَ
Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba!
خَلَقَ ٱلۡإِنسَٰنَ مِنۡ عَلَقٍ
Amemuumba binaadamu kwa tone la damu!
ٱقۡرَأۡ وَرَبُّكَ ٱلۡأَكۡرَمُ
Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote!
ٱلَّذِي عَلَّمَ بِٱلۡقَلَمِ
Ambaye amefundisha kwa kalamu.
عَلَّمَ ٱلۡإِنسَٰنَ مَا لَمۡ يَعۡلَمۡ
Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui.
كَلَّآ إِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ لَيَطۡغَىٰٓ
Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri.
أَن رَّءَاهُ ٱسۡتَغۡنَىٰٓ
Akijiona katajirika.
إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلرُّجۡعَىٰٓ
Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo.
أَرَءَيۡتَ ٱلَّذِي يَنۡهَىٰ
Umemwona yule anaye mkataza.
عَبۡدًا إِذَا صَلَّىٰٓ
Mja anapo sali?
أَرَءَيۡتَ إِن كَانَ عَلَى ٱلۡهُدَىٰٓ
Umeona kama yeye yuko juu ya uwongofu?
أَوۡ أَمَرَ بِٱلتَّقۡوَىٰٓ
Au anaamrisha uchamngu?
أَرَءَيۡتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰٓ
Umeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma?
أَلَمۡ يَعۡلَم بِأَنَّ ٱللَّهَ يَرَىٰ
Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona?
كَلَّا لَئِن لَّمۡ يَنتَهِ لَنَسۡفَعَۢا بِٱلنَّاصِيَةِ
Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele!
نَاصِيَةٖ كَٰذِبَةٍ خَاطِئَةٖ
Shungi la uwongo, lenye makosa!
فَلۡيَدۡعُ نَادِيَهُۥ
Basi na awaite wenzake!
سَنَدۡعُ ٱلزَّبَانِيَةَ
Nasi tutawaita Mazabania!
كَلَّا لَا تُطِعۡهُ وَٱسۡجُدۡۤ وَٱقۡتَرِب۩
Hasha! Usimt'ii! Nawe sujudu na ujongee!