Skip to content
فُصِّلَت /

Aya 40

41 : 40

Aya 40 of فُصِّلَت (41 : 40). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

فُصِّلَت Aya 54
Sura · فُصِّلَت
Kiswahili · Barawani
41 : 40

إِنَّ ٱلَّذِينَ يُلۡحِدُونَ فِيٓ ءَايَٰتِنَا لَا يَخۡفَوۡنَ عَلَيۡنَآۗ أَفَمَن يُلۡقَىٰ فِي ٱلنَّارِ خَيۡرٌ أَم مَّن يَأۡتِيٓ ءَامِنٗا يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ ٱعۡمَلُواْ مَا شِئۡتُمۡ إِنَّهُۥ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٌ

Hakika wale wanao upotoa ukweli uliomo katika Ishara zetu hawatufichikii Sisi. Je! Atakaye tupwa Motoni ni bora au atakaye kuja kwa amani Siku ya Kiyama? Tendeni mpendavyo, kwa hakika Yeye anayaona mnayo yatenda.

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika hao wanao iacha Njia iliyo sawa kwa mintarafu ya Ishara zetu na wakaitupilia mbali kwa kuikadhibisha, mambo yao hayatupotei Sisi wala hayo wanayo yakusudia. Nasi tutawalipa kama wanavyo stahiki. Kwani anaye tupwa katika Moto ni bora au yule anaye kuja naye hali katulia Siku ya Kiyama kwa kuokoka kwake na kila ovu? Kabisa hao hawalingani. Waambie kwa kuwaahidi: Fanyeni mtakavyo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuzunguka kila kitu kwa jicho lake, naye atamlipa kila mmoja kwa a'mali yake.