41 : 33
وَمَنۡ أَحۡسَنُ قَوۡلٗا مِّمَّن دَعَآ إِلَى ٱللَّهِ وَعَمِلَ صَٰلِحٗا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ ٱلۡمُسۡلِمِينَ
Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema, na akasema: Hakika mimi ni katika Waislamu?
Explanation & meanings · 1
- Hapana mwenye kauli nzuri zaidi kuliko mwenye kulingania Tawhid ya Mwenyezi Mungu na ut'iifu wake, na pamoja na hayo, akatenda vitendo vyema, na akasema kwa kuungama itikadi yake: Hakika mimi ni miongoni mwa Waislamu, yaani wenye kunyenyekea amri za Mwenyezi Mungu.