Skip to content
فُصِّلَت /

Aya 15

41 : 15

Aya 15 of فُصِّلَت (41 : 15). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

فُصِّلَت Aya 54
Sura · فُصِّلَت
Kiswahili · Barawani
41 : 15

فَأَمَّا عَادٞ فَٱسۡتَكۡبَرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ بِغَيۡرِ ٱلۡحَقِّ وَقَالُواْ مَنۡ أَشَدُّ مِنَّا قُوَّةًۖ أَوَلَمۡ يَرَوۡاْ أَنَّ ٱللَّهَ ٱلَّذِي خَلَقَهُمۡ هُوَ أَشَدُّ مِنۡهُمۡ قُوَّةٗۖ وَكَانُواْ بِـَٔايَٰتِنَا يَجۡحَدُونَ

Ama kina A'di walijivuna katika nchi bila ya haki, na wakasema: Nani aliye kuwa na nguvu kushinda sisi? Kwani wao hawakuona kwamba Mwenyezi Mungu aliye waumba ni Mwenye nguvu kushinda wao? Na wao wakawa wanazikataa Ishara zetu!

Explanation & meanings · 1
  1. Ama kina A'di walipandwa na kiburi katika nchi bila ya haki ya kuwa na kiburi hicho. Na walisema kwa kughurika na nafsi zao: Nani huyo anaye tushinda sisi kwa nguvu? Ama ajabu watu hawa! Wanasema hayo na wao hawaoni kwamba Mwenyezi Mungu aliye waumba ana nguvu zaidi kuwashinda wao? Na wao walikuwa wakizikanya Ishara zetu!