41 : 26
وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَا تَسۡمَعُواْ لِهَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانِ وَٱلۡغَوۡاْ فِيهِ لَعَلَّكُمۡ تَغۡلِبُونَ
Na walio kufuru walisema: Msiisikilize Qur'ani hii, na timueni zogo, huenda mkashinda.
Explanation & meanings · 1
- Makafiri wakaambizana wenyewe kwa wenyewe: Msiisikilize hii Qur'ani, na inapo somwa nyie leteni porojo lisio kuwa na maana, ili pasiwepo mtu wa kuisikia wala kunafiika kwayo, asaa kwa hivyo mkamshinda Muhammad.