Skip to content

utakapo ulizwa: ni ipi maana ya shahada kuwa hapana Mungu apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mungu mmoja na kwamba Muhammad nimtume wa Mwenyezi Mungu?

السؤال

Swali/ utakapo ulizwa: ni ipi maana ya shahada kuwa hapana Mungu apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mungu mmoja na kwamba Muhammad nimtume wa Mwenyezi Mungu?

الجواب

Jawabu/ sema: Shahada kuwa hapana Mungu apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu: Maana yake: Hakuna wa kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu kama ilivyo katika kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na pale Ibrahim alipo mwambia baba yake na kaumu yake: Hakika mimi ninajitenga mbali na hayo mnayo yaabudu. (26) Isipo kuwa yule aliye niumba, kwani Yeye ataniongoa.(27) Na akalifanya hili liwe neno lenye kubaki katika vizazi vyake ili warejee}.(Zukhruf26-28) na amesema Mwenyezi Mungu:{ Kwani huoni kwamba Mwenyezi Mungu huuingiza usiku katika mchana na huuingiza mchana katika usiku na amedhalilisha jua na mwezi? Vyote hivyo vinakwenda mpaka wakati ulio wekwa. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayo yatenda}. (Luqman 29)

Na maana ya Shahada ya kuwa muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu: Ni kuyakinisha yakwamba ni mja wa Mwenyezi Mungu na nimtume wake na kwamba yeye ni mtumwa haabudiwi na ni mtume hakadhibishwi, anatiiwa kwa yale aliyo yaamrisha na anasadikishwa kwa yale aliyo yaeleza na yanatengwa mbali yale yote aliyo yakataza na kuyakemeya na asiabudiwe Mwenyezi Mungu ila kwa sheria yake bila kuzidisha wala kupunguza.

Na haki ya Mtume rehma na amani ziwe juu yake juu ya Ummah wake, ni kumuheshimu na kumtukuza na kumpenda na kumfuata, katika kila wakati na zama kwa kadri ya uwezo, amesema Mwenyezi Mungu: {Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu.} (Al Imran 31)