Utakapo ulizwa: Ni zipi aina za Tawhiid?
السؤال
Swali/ Utakapo ulizwa: Ni zipi aina za Tawhiid?
الجواب
Jawabu/ Sema: Tawhiidi ina vigawanyo vitatu: 1. Tawhiid Rububiyyah: nayo ni kuitakidi kwa mkato kwamba Mwenyezi Mungu ndie muumbaji anae toa rizki na mwenye kupangikia mambo ya waja wake wote, hana Mshirika wala msaidizi na yo ni kumkwekesa Mwenyezi Mungu kwa vitendo vyake Allah, anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:{Ati yupo muumba mwengine asiye kuwa Mwenyezi Mungu anaye kupeni riziki kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Hapana mungu ila Yeye tu. Basi wapi mnako geuzwa?} (Fatwir 3) na anasema Mwenyezi Mungu: {Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti}. (adh-adhariyat 58) na anasema Mwenyezi Mungu: {Anapitisha mambo yote yalio baina mbingu na ardhi} (Asajidah 5) na amesema Mwenyezi Mungu: {Fahamuni! Kuumba na amri ni zake. Ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.} (Al-Aaraf 54).
- Tawhiidul Asmaai wa swifati: nayo ni kuitakidi kwamba Mwenyezi Mungu ana majina mazuri na sifa zilizo kamilika zilizo thibiti katika Qur'an na sunnahh, bila kufananisha wala kulinganisha, wala kupindisha wala kugeuza na kwamba Mwenyezi Mungu hana mfano wa kitu chochote, amesema Mwenyezi Mungu mtukufu: { Hana mfano wa chochote na yeye nimsikivu na anaona} ( Shura 11). na amesema Mwenyezi Mungu: {Mwenyezi Mungu ana majina mazuri muombeni kupitia majina hayo}.
3. Tawhiid Al-Uluhiyyah: nayo ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu pekeyake hana mshirika katika ibada, yaani kumpwekwsha Mwenyezi Mungu katika vitendo vya waja wake inaitwa tawhiidi ya kiibada, amesema Mwenyezi Mungu: {Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia dini} (Albayyinah5) na amesema Mwenyezi Mungu:{ Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote ila tulimfunulia ya kwamba hapana mungu isipo kuwa Mimi. Basi niabuduni Mimi tu} (Al-Anbiyaai 25) na mgawanyo huu ni kwajili ya kuweka wazi maswala ya kielimu na kama sio hivyo huo mgawanyo unalazima kuwepo katika itikadi ya kila Muislam mwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu na mwnye kufuata Kitabu na sunnahh.