Skip to content

Utakapo ulizwa: Je, Mwanadamu anaendeshwa katika mambo yote anayo yafanya au amekhiyarishwa?

السؤال

Swali/ Utakapo ulizwa: Je, Mwanadamu anaendeshwa katika mambo yote anayo yafanya au amekhiyarishwa?

الجواب

Jawabu/ Sema: Haisemwi kuwa Mwanadamu anaendeshwa katika mambo yote au amekhiyarishwa yote mawili ni makosa, dalili za kitabu na sunnahh zimeonyesha kuwa mwanadamu ana utashi wake na kwamba yeye ndie mtendaji kwa uhakika wake, lakini yote hayo hayatoki katika elimu ya Mwenyezi Mungu utashi wake, kinacho bainisha hayo ni kauli ya mwenyezi Mungu: {Kwa mwenyekutaka miongoni mwenu, kulingana na kushikamana juu ya haki na Imani(28) Wala nyinyi hamtotaka isipokuwa kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe wote} (Takwiir 28-29) na amesema Mwenyezi Mungu: {Mwenye kutaka ataizingatia(55) na hawata zingatia na kuwaidhika ila akitaka Mwenyezi Mungu yeye ndie anae stahiki kuogopwa na yeye ndie anaestahiki kusamehe} (Mudathir 55-56)