Utakapo ulizwa: Je, Dua ni katika Ibada?
السؤال
Swali/ Utakapo ulizwa: Je, Dua ni katika Ibada?
الجواب
Jawabu/ Sema: Hakika Dua ni katika aina kubwa ya ibada, kama alivyo sema Allah mtukufu: {Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni. Kwa hakika wale ambao wanajivuna na kuniabudu Mimi wataingia Jahannamu wadhalilike} (Ghafir 60) na katika hadithi: Amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Dua ndio Ibada) Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy na kwa ukubwa wa dua na umuhimu wake katika dini imekuja dua katika zaidi ya aya mia tatu (300) katika Qur'an Tukufu na dua ina aina mbili:dua ya ibada na dua ya Maombi na kila kimoja hakitimii mpaka kiwe na mwenzake.
Dua ya ibada: Ni kujikurubisha kwa Allah mtukufu kwa ajili ya kupata unacho kitafuta, au kuzuia mabaya, au kuondoa madhara kwa kufanya ikhlas katika ibada za Allah mtukufu. Anasema Allah Mtukufu: {Na Dhun-Nun alipoondoka hali ameghadhibika na akadhani ya kwamba hatutakuwa na uwezo juu yake. Basi aliita katika giza: Hapana mungu isipo kuwa Wewe Subhanaka Uliye takasika. Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu (87) Basi tukamwitikia na tukamwokoa kutokana na dhiki. Na hivyo ndivyo tunavyo waokoa Waumini} (Al-Anbiyaa 87-88).
Dua ya Maombi: ni kuomba mambo yenye manufaa kwa muombaji miongoni mwa kuleta manufaa, au kuondoa madhara. Amesema Allah Mtukufu: {Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tumeamini, basi tufutie madhambi yetu na tuepushe na adhabu ya Moto} (Al-Imran 16)
Dua kwa aina zake mbili ndio ubongo wa ibada kwa uchache wake nayo ni ibada nyepesi kwa kuiomba na ndiyo yenye cheo cha juu na athari kubwa, dua ni sababu yenye nguvu katika kuzuia mambo mabaya na mtu kupata kile anacho kitafuta kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.