utakapo ulizwa: ni yapi masharti ya kukubaliwa ibada kwa Allah Mtukufu?
السؤال
Swali/ utakapo ulizwa: ni yapi masharti ya kukubaliwa ibada kwa Allah Mtukufu?
الجواب
Jawabu/ Sema: Ibada haikubaliwi kwa Allah mpaka itimize masharti mawili: Sharti la kwanza: Ibada iwe kwa ajili ya Allah mtukufu na ushahidi ni Kauli yake Mwenyezi Mungu: {Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia dini} (Albayyinah 5) na amesema Mwenyezi Mungu mtukufu: {Mwenye kutaraji kukutana na Mola wake Mlezi basi naatende vitendo vyema, wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake Mlezi} (Kahfi 110)
Sharti la pili: Iwe ibada ni yenye kuafikiana na sheria aliyo kujanayo Mtume rehma na amani ziwe juu yake na dalili ni kauli ya Mwenyezi Mungu mtukufu: {Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu} (Al-Imran31). na kauli ya Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Mwenyekufanya ibada ambayo haipo katika dini yetu basi atarudishia mwenyewe) Imepokelewa na Imamu Muslim. na kama ibada haikubaliani na uongofu wa Mtume rehma na amani ziwe juu yake hakika ibada hiyo haikubaliwi hatakama alie ifanya ameifanya kwa ajili ya Allah.