Skip to content

Utakapo ulizwa: Kuamini Hukumu ya Mwenyezi Mungu na Qadar zake inakuwa vipi?

السؤال

Swali/ Utakapo ulizwa: Kuamini Hukumu ya Mwenyezi Mungu na Qadar zake inakuwa vipi?

الجواب

Jawabu/ Sema: Inakuwa kwa yakini ya mkato kwamba kila kitu kinakuwa kwa hukumu ya Mwenyezi Mungu na mipangilio yake, hakiwi kitu chochote ila kwa utashi wake, yeye ndie alie umba vitendo vya waja wake vya heri na shari, na akawaumba waja wake katika maumbile ya heri na ya kukubali haki, na akawapa akili yenye kupambanua na akawaruzuku utashi ambao watachagua wanacho kipenda kwa utashi huo, na akawabainishia haki na akawatahadhalisha na batili, akamuongoza anae mtaka kwa fadhila zake na akampoteza anae mtaka kwa uadilifu wake, yeye ndie mwenye hekima na ni mjuzi mwenye huruma, haulizwi kwa anacho kifanya na waja wanaulizwa kwa kila wanacho kifanya.

Daraja za Qadar ni nne:

Daraja ya kwanza: Ni kuamini elimu ya Mwenyezi Mungu kwamba yeye amekizunguka kila kitu, yeye ni mjuzi kwa yale yalio tokea na yale yanayo tokea na yale ambayo hayajatokea, kama yangetokea yangekua vipi.

Daraja la pili: Ni kuamini kwamba Mwenyezi Mungu aliandika kila kitu.

Daraja la tatu: Ni kuamini kwamba kwa Mwenyezi Mungu hakiwi chochote ila kwa utashi wake.

Daraja la nne: Ni kuamini kwamba Mwenyezi Mungu ndie alie umba kila kitu, yeye ndie alie umba dhati ya vitu na matendo na maneno na harakati na utulivu na sifa na kila kitu katika ulimwengu wa juu na wachini na wa aridhini, na dalili za yalio tangulia ziku nyingi katika kitabu cha Mwenyezi Mungu na suna za Mtume.