Skip to content

Utakapo Ulizwa: Je Adhabu za kaburi na neema zake zimethibiti katika Qur'an na sunnah?

السؤال

Swali/ Utakapo Ulizwa: Je Adhabu za kaburi na neema zake zimethibiti katika Qur'an na sunnah?

الجواب

Jawabu/ Sema: Ndio, amesema Mwenyezi Mungu mtukufu: {Wanaonyeshwa Moto asubuhi na jioni. Na itapo fika Saa ya Qiyama patasemwa: Waingizeni watu wa Firauni katika adhabu kali kabisa!} (Ghafir 46) na amesema Mwenyezi Mungu: {Na laiti ungeli ona Malaika wanapo wafisha wale walio kufuru wakiwapiga nyuso zao na migongo yao na kuwaambia: Ionjeni adhabu ya Moto!} (Anfal 50) na kauli ya Mwenyezi Mungu: {Mwenyezi Mungu huwatia imara wenye kuamini kwa kauli ya imara katika maisha ya dunia na katika akhera} (Ibrahim 27) na imekuja katika hadithi Qudsiy ndefu kutoka kwa swahaba Baraa -radhi za Allah ziwe juu yake-: (Atanadi mwenye kunadi mbinguni akisema: Amesema ukweli mjawangu mtandikieni peponi na mumvishe mavazi ya watu wa peponi na mfungulieni mlango wa pepo, inatoka katika pepo hiyo harufu nzuri kisha kaburi lake linapanuliwa, inakuwa kubwa kiasi cha upeo wa macho yake na hakika kafiri, kisha akataja hali anayo ipata wakati wa kufa kwake, akasema: Kisha roho yake inarejeshwa katika mwili wake, kisha wanamjia malaika wawili, kisha wanamkalisha, kisha wanamuuliza: Nani mola wako? atajibu: haa haa sijuwi, kisha wanamuuliza ni ipi dini yako? atajibu haa haa sijuwi, kisha watamuuliza niyupi huyo mwanaume alie tumwa kwenu? atajibu: haa haa sijuwi, atanadi mwenye kunadi mbinguni akisema: huyo amesema uwongo mtandikieni matandiko ya motoni na mvisheni mavazi ya watu wa motoni na mfungulieni mlango wa moto, kisha ule moto na joto na sumu zake vinamjia, kisha kaburi linambana mpaka mbavu zake zinatofautiana. Amezidisha mpokezi katika riwaya: (Kisha analetewa malaika asie ona wala hazungumzi, akiwa na nyundo kubwa na nzito ya chuma, laiti ungepigwa mlima kwa nyundo hiyo mlima ungesagika ukawa kama mchanga, kisha anapigwa nayo pigo moja ambalo viumbe vyote vya mashariki na magharibi vinasikia ila watu na majini hawasikii). Imepokelewa na Abudaud. Kwa sababu ya jambo hili ndio maana Mtume akatuamrisha tujilinde kwake na adhabu za kaburini katika kila swala.