Skip to content

Utakapo ulizwa: Ni yapi masharti ya Lailaha ila Allah?

السؤال

Swali/ Utakapo ulizwa: Ni yapi masharti ya Lailaha ila Allah?

الجواب

Jawabu/ Sema: Neno la tawhiid halitoshi kutamkwa bila ya kuitakidi na kuzingatia na kusimamia mambo yanayo pelekea kutamka neno hilo na kujiepusha na mambo yanayo yatengua, bali neno hilo lina masharti saba, wanachuoni wameyatoa masharti hayo katika dalili ya kisheria, wakaziandika na kuzitolea dalili katika Qur'an na Sunnah nazo:

1- Elimu kwa maana yake katika kukanusha na kuthibitisha, ni kujua kuwa hakika Mwenyezi Mungu hana mshirika na yeye ndie anaestahiki kuabudiwa na dalili ambazo zimeonyesha kukanusha Uungu kwa asiekuwa Mwenyezi Mungu na kujua mambo ya lazima na yanayo takiwa kufanywa baada ya kutamka neno hilo pia nakujua mambo yanayo batilisha neno hilo, amesema Mwenyezi Mungu mtukufu: {Basi jua ya kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu} (muhammad 19) na amesema Mwenyezi Mungu: { isipo kuwa anaye shuhudia kwa haki na wao wanajua} (Zukhruf 86), amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: Atakae kufa akiwa anajua kuwa hakuna Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Allah ataingia peponi) Imepokelewa na Imamu muslim.

2- Yakini nayo: nikuitakidi kwa mkato juu ya neno hilo la shahada, yakini ambayo inayo pingana na Shaka au wasiwasi, yakini ilio thibiti katika moyo, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: { Hakika Waumini ni wale walio muamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake tena wasitie shaka kabisa na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao. Hao ndio wakweli}(Al-Hujrat 15) na amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Atakae sema ninashahidilia kuwa hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Mwenyezi Mungu na mimi ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu mja hakutani na Mwenyezi Mungu akiwa na shahada hizo mbili bila ya kuwa na mashaka katika hizo shahada ila ataingia peponi) Imepokelewa na Muslim.

3.Ikhlasi inayo pinga Ushirikina, kwasababu ya kusafisha Ibada na kuitakatisha kutokana na uchafu wa ushirikina, au kujionyesha. Amesema Allah mtukufu: {Hakika dini Safi ni ya Mwenyezi Mungu tu.} ( Zumar 3) na amesema Allah mtukufu: {Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia dini} (Albayyinah 5) na amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: ( Watu watakao pata mafanikio ya uombezi wangu siku ya Qiyama, ni mtu aliesema Lailaha ila Allah akiwa na Ikhlas katika moyo wake na nafsi yake) Imepokelewa na Imamu Bukhary.

4. Mapenzi (Mahaba) ya neno hilo la tawhiid na yale ambayo yanayo elezwa na neno hilo, na kufurahia hilo, na kuwapenda wenye kulisema neno hilo, na kukithirisha mapenzi kwao, na kuwachukia wanao lipinga neno hilo na kujitenga mbali nao wakiwemo makafiri, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:,{Na katika watu wapo wanao chukua waungu wasio kuwa Mwenyezi Mungu. Wanawapenda kama kumpenda Mwenyezi Mungu. Lakini walio amini wanampenda Mwenyezi Mungu zaidi sana} (Albaqara 165) na amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Mambo matatu atakae kuwa nayo atapata utamu wa imani, awe Allah na Mtume wake ndio vipenzi vyake kuliko vitu vyote, na ampende mtu hampendi kwa lolote ila ni kwa ajili ya Allah, na achukie kurudi katika ukafiri kama anavyo chukia kutupwa Motoni) Imepokelewa na Imamu Muslim.

5. Ukweli unao pingana na Uwongo na ukweli unakuwa kwa Moyo kuafikiana na viungo katika kile kilicho tamkwa na ulimi ambacho ni neno la Tawhiid, viungo vinasadikisha moyo kwa maneno yaliyo semwa na moyo huo vinafanya Ibada za wazi na za ndani, Amesema Allah mtukufu:{Mwenyezi Mungu atawatambulisha walio wa kweli na atawatambulisha walio waongo} (Al-Ankabuti 3) na amesema Allah Mtukufu: {Na aliye ileta Kweli na akaithibitisha - hao ndio wachamngu} (Azzumar 33) na amesema Mtume rehma na amani ziwe juu yake: (Atakae kufa akiwa anashahidilia kuwa Hapana Mungu apasae kuabudiwa kwa haki na Muhammad ni mtume wa Allah akiwa ni mkweli katika moyo wake ataingia peponi) Imepokelewa na Imamu Ahmad.

6. Kuzingatia, kwa kunyenyekea kwa ajili ya Allah kwa kumpwekesha katika ibada na kuleta haki zake kwa kutekeleza maamrisho yake nakujiepusha na makatazo yake kwa Ikhlasi kutaka thawabu na kutarajia malipo kwa Allah na kwa kumuogopa Allah, Amesema Allah mtukufu: {Na rejeeni kwa Mola wenu Mlezi na silimuni kwake} (Zumar 54) na amesema Allah Mtukufu {Na mwenye kuuelekeza uso wake kwa Mwenyezi Mungu naye akawa anafanya wema, basi huyo hakika amekwisha kamata fundo lilio madhubuti} (Luqman 22)

  1. Kukubali kunako pingana na kukataa na inakuwa kwa moyo kukubali neno la tawhiid na yale yanayo patikana katika tamko hilo, lakini neno hilo halipokelewi kwa mwenye kujidai kufuata neno hilo kwa kujibaguwa na wengine au kwa kiburi, Anasema Allah mtukufu: { Wao walipo kuwa wakiambiwa La ilaha illa 'Llahu Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu tu, wakijivuna} (Swafati 35). Huyo hawi muislam