Skip to content

Mwenyezi Mungu akimpangia mja afie sehemu fulani humfanya ahitajie kitu sehemu ile

Imepokelewa kutoka kwa Matwar Bin Ukaamis -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-

"Mwenyezi Mungu akimpangia mja afie sehemu fulani humfanya ahitajie kitu sehemu ile."

«إِذَا قَضَى اللَّهُ لِعَبْدٍ أَنْ يَمُوتَ بِأَرْضٍ جَعَلَ لَهُ إِلَيْهَا حَاجَةً».

Imepokelewa Imamu Tirmidhiy
Sahihi
Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: kuwa Mwenyezi Mungu akimpangia mtu kuwa afie katika ardhi fulani na hali yakuwa yeye hayupo katika ardhi hiyo; Basi humfanya ahitajie kitu katika ardhi ile hivyo ataenda katika ardhi ile, basi huchukuliwa roho yake akiwa huko.

Maana ya Maneno

...:

Katika Faida za Hadithi

Hadithi inathibitisha maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na nafsi haijui itafia katika ardhi gani."

Rejea

Sunanu Tirmidhiy (4/ 23) (2146).

Zaidi (1)

تحفة الأحوذي (6/ 299).