Skip to content
Orodha ya Sura /

القَدر

القَدر is chapter 97 of the Quran and has 5 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

5 Aya Sura Na. 97
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

إِنَّآ أَنزَلۡنَٰهُ فِي لَيۡلَةِ ٱلۡقَدۡرِ

Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani katika Laylatul Qadri, Usiku wa Cheo Kitukufu.

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani katika usiku wa Cheo na Utukufu.

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا لَيۡلَةُ ٱلۡقَدۡرِ

Na nini kitacho kujuulisha nini Laylatul Qadri?

Explanation & meanings · 1
  1. Na kitu gani kitakufunza ni nini usiku huo wa Cheo na Utukufu?

لَيۡلَةُ ٱلۡقَدۡرِ خَيۡرٞ مِّنۡ أَلۡفِ شَهۡرٖ

Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu.

Explanation & meanings · 1
  1. Usiku wa Qadr na Sharaf, Cheo na Utukufu, ni bora kuliko miezi elfu, kwa kuwa umekhusika kwa kuteremka ndani yake Qur'ani tukufu.

تَنَزَّلُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ وَٱلرُّوحُ فِيهَا بِإِذۡنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ أَمۡرٖ

Huteremka Malaika na Roho katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa kila jambo.

Explanation & meanings · 1
  1. Huteremka Malaika na Jibrili katika usiku huo mpaka kwenye ardhi kwa idhini ya Mola wao Mlezi kwa sababu ya kila jambo.

سَلَٰمٌ هِيَ حَتَّىٰ مَطۡلَعِ ٱلۡفَجۡرِ

Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri.

Explanation & meanings · 1
  1. Na wameaminika na maudhi na uovu. Hali inabaki hivyo mpaka mapambazuko ya alfajiri.