Skip to content
النِّسَاء /

Aya 103

4 : 103

Aya 103 of النِّسَاء (4 : 103). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

النِّسَاء Aya 176
Sura · النِّسَاء
Kiswahili · Barawani
4 : 103

فَإِذَا قَضَيۡتُمُ ٱلصَّلَوٰةَ فَٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ قِيَٰمٗا وَقُعُودٗا وَعَلَىٰ جُنُوبِكُمۡۚ فَإِذَا ٱطۡمَأۡنَنتُمۡ فَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَۚ إِنَّ ٱلصَّلَوٰةَ كَانَتۡ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ كِتَٰبٗا مَّوۡقُوتٗا

Mkisha sali basi mkumbukeni Mwenyezi Mungu mkisimama, na mkikaa, na mnapo jinyoosha kwa kulala. Na mtapo tulia basi shikeni Sala kama dasturi. Kwani hakika Sala kwa Waumini ni faradhi iliyo wekewa nyakati maalumu.

Explanation & meanings · 1
  1. Na mkisha Swala ya vita, inayo itwa Swala ya Khofu, msisahau kumkumbuka Mwenyezi Mungu daima. Mkumbukeni nanyi mmesimama, mnapigana, mmekaa, na mmelala. Kwani kumkumbuka Mwenyezi Mungu Mtukufu kunatia nguvu nyoyo, na kuzituliza. Khofu ikiondoka pakawa na utulivu basi timizeni Swala kwa ukamilifu, kwani Swala imefaridhiwa juu ya Waumini isaliwe kwa nyakati zake.