Skip to content
An-Nisa /

Aya 104

4 : 104

Aya 104 of An-Nisa (4 : 104). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

An-Nisa Aya 176
Sura · An-Nisa
Kiswahili · Barawani
4 : 104

وَلَا تَهِنُواْ فِي ٱبۡتِغَآءِ ٱلۡقَوۡمِۖ إِن تَكُونُواْ تَأۡلَمُونَ فَإِنَّهُمۡ يَأۡلَمُونَ كَمَا تَأۡلَمُونَۖ وَتَرۡجُونَ مِنَ ٱللَّهِ مَا لَا يَرۡجُونَۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمًا

Wala msifanye ulegevu kuwafukuzia kaumu ya maadui. Ikiwa mnaumia, basi nao pia wanaumia kama mnavyo umia nyinyi. Nanyi mnataraji kwa Mwenyezi Mungu wasio yataraji wao. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye hikima.

Explanation & meanings · 1
  1. Msilegee kuwafukuzia makafiri walio kwisha kukutangazieni vita na wanajaribu kukushambulieni kila pahala. Hakika vita havikosi maumivu. Ikiwa nyinyi Waumini mmepata majaraha na mengineyo, na wao makafiri pia wameyapata machungu. Khitilafu yenu ni kuwa wao hawapiganii Haki, wala hawataraji kitu kwa Mwenyezi Mungu; na nyinyi mnataka Haki na mnataraji radhi za Mwenyezi Mungu na neema za kudumu. Na Mwenyezi Mungu anavijua vitendo vyenu na vyao, naye ni Mwenye hikima, anamlipa kila mtu kwa alitendalo.