Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 56 kati ya 839

Ondoa vichujio
"Laiti nyinyi mgetegemea kwa Mwenyezi Mungu ukweli wa kumtegemea, basi angekuruzukuni kama anavyowaruzuku ndege, wanatoka asubuhi wakiwa na njaa, wanarudi jioni wakiwa wameshiba".
Sahihi Imepokelewa na Imam Ahmad, Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na Ibn Hibban katika Sahih yake na Haakim
"Mwenyezi Mungu alipoumba Pepo na Moto alimtuma Malaika Jibril -Amani iwe juu yake- aende peponi Akamwambia: Iangalie hiyo pepo na yale niliyo waandalia humo watu wa peponi, basi Jibrili akaiangalia Pepo kisha akarudi, akasema: Naapa kwa utukufu Wako ewe Mwenyezi Mungu hatozisikia mtu yeyote habari za pepo kisha asiingie humo, kisha akamuamrisha kuizungushia Pepo hiyo mambo yenye kuchukiza, kisha akamwambia nenda tena ukaiangalie na uangalie yale niyowaandalia watu wake humo peponi. Basi akaiangalia ghafla akaiona imezungushwa vyenye kuchukiza, akasema: Naapa kwa utukufu Wako kwa hakika ninahofia kuwa hatoingia mtu yeyote. Akasema kumwambia Jibrili nenda na uuangalie Moto na yale niliyo waandalia humo watu wa Motoni. Basi akauangalia Moto na akauona Moto ulivyopambwa, basi akarudi na akasema: Naapa kwa utukufu Wako hatoingia yeyote humo, basi akaamrisha ukazungushwa mambo yenye kutamanisha, basi akamwambia: Rudi na uuangalie tena. Basi akauangalia akaukuta umepambwa na kuzungushwa yenye kutamanisha, basi akarudi na akasema: Naapa kwa utukufu wako kwa hakika nahofia yakuwa hatosalimika mtu yeyote isipokuwa ataingia Motoni."
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na Nasaai
"Mwenye kuisoma Qur'ani kwa sauti ya wazi ni kama mwenye kutoa sadaka hadharani, na mwenye kuisoma Qur'ani kwa siri ni kama mwenye kuficha sadaka."
Sahihi Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na Nasaai
"Mahala pa karibu zaidi anapokuwa Mola Mlezi na mja ni katikati ya usiku wa mwisho, ikiwa utaweza kuwa miongoni mwa wanaomtaja Mwenyezi Mungu katika wakati huo basi fanya".
Sahihi Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na Nasaai
Walinieleza watu wawili kuwa wao walimjia Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika Hija ya kuaga wakati akigawa sadaka, wakamuomba katika sadaka hizo, akatunyanyulia macho kisha akayashusha, akatuona ni watu shupavu wenye nguvu, akasema: "Ikiwa mtapenda nitakupeni, lakini mali hii tajiri hana fungu ndani yake wala mwenye nguvu mwenye uwezo wa kuchuma mali".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud na Nasai
Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake akasema: Wasemaje kuhusu mtu aliyepigana vita akitaka malipo kwa Allah na kusemwa vizuri na watu, ana lipi? Akasema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Hana malipo yoyote" Akalirudia hilo mara tatu, akimwambia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Hana malipo yoyote" Kisha akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu hakubali amali yoyote isipokuwa ile itakayokuwa imetakasiwa nia, na ikakusudiwa kupata radhi za Allah (na kwenda kuuona uso wake)".
Sahihi Imepokelewa na An-nasaiy
Tulitoka katika usiku wa mvua kubwa na giza nene, tukimtafuta Mtume rehema na amani ziwe juu yake; ili atusalishe, anasema: Nikampata, akasema: "Sema" Nikawa sikusema kitu, kisha akasema: "Sema", Nikawa sikusema kitu, akasema: "Sema" Nikasema: Niseme nini? Akasema: "Sema Yeye ni Mwenyezi Mungu mmoja tu" na sura mbili za kinga unapofika nyakati za jioni na nyakati za asubuhi mara tatu, zitakutosheleza kila kitu".
Sahihi Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na Nasaai
"Dhikiri bora ni: Laa ilaaha Illa llaah: Na dua bora ni: Al-hamdulillah".
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn Majah