Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 8 kati ya 839

Ondoa vichujio
"Laiti wangepewa watu yote wanayodai basi kuna watu wangedai mali za wenzao na damu zao, lakini ushahidi ni kwa mwenye kudai na kiapo ni kwa mwenye kukanusha".
Sahihi Imepokelewa na Albayhaqy
Katika sunna atakaposema muadhini katika adhana ya Alfajiri: Hayya Alal-fala'h, aseme: Aswalatu khairu mmina nnaum. Yaani: Swala ni bora kuliko usingizi.
Sahihi Imepokelewa na Ibnu Khuzaymah, Addar- Alqutni na Albayhaqy
"Laiti wangelipewa watu yote wanayodai basi kuna watu wangedai mali za wenzao na damu zao, lakini ushahidi ni kwa mwenye kudai na kiapo ni kwa mwenye kukanusha".
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Baihaqiy na wengineo hivi na baadhi yake iko katika Swahihi mbili.
"Hakika Mwenyezi Mungu ameniondolea mimi kwa umma wangu (madhambi ya) kukosea na kusahau, na yale waliyolazimishwa".
Amesema Imamu Nawawi: Hadithi hii ni hasan Imepokelewa na Ibnu Maajah, Al-Bayhaqi na wengineo.
"Peaneni zawadi, mtapendana."
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Bukhari katika Al-Adab Al-Mufrad na Abuu Ya'laa na Al-Bayhaqiy.
"Liepukeni chafu hili alilolikataza Mwenyezi Mungu, atakayetumbukia katika hilo basi ajifiche kwa stara ya Mwenyezi Mungu na atubie kwa Mwenyezi Mungu, kwa sababu atakayetufungulia ukurasa wake tutamsimamishia kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu".
Sahihi Imepokelewa na Hakim na Bayhaqy
Hakuwahi kuwapiga vita Mtume rehema na amani ziwe juu yake watu hata siku moja isipokuwa kwanza alianza kuwaita katika Uislamu.
Sahihi Imepokelewa na Ahmad na Albayhaqy
"Kwa hakika nimetumwa ili kutimiliza tabia njema"
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Al-Bukhari katika Al-Adab Al-Mufrad na Ahmad na Al-Bayhaqi