Skip to content
المَائدة /

Aya 23

5 : 23

Aya 23 of المَائدة (5 : 23). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

المَائدة Aya 120
Sura · المَائدة
Kiswahili · Barawani
5 : 23

قَالَ رَجُلَانِ مِنَ ٱلَّذِينَ يَخَافُونَ أَنۡعَمَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمَا ٱدۡخُلُواْ عَلَيۡهِمُ ٱلۡبَابَ فَإِذَا دَخَلۡتُمُوهُ فَإِنَّكُمۡ غَٰلِبُونَۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَتَوَكَّلُوٓاْ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Watu wawili miongoni mwa wachamngu ambao Mwenyezi Mungu amewaneemesha, walisema: Waingilieni kwa mlangoni. Mtakapo waingilia basi kwa yakini nyinyi mtashinda. Na mtegemeeni Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni Waumini.

Explanation & meanings · 1
  1. Wawili kati ya wakubwa wao walio kuwa wanamwogopa Mwenyezi Mungu, na ambao Mwenyezi Mungu amewapa neema ya imani na ut'iifu, walisema: Enyi watu! Waingilieni hao majabari wa mjini kwa kupitia mlangoni kwa ghafla. Mkifanya hivyo nyinyi mtawashinda. Na mtegemeeni Mwenyezi Mungu peke yake katika mambo yenu yote, ikiwa nyiny ni wenye Imani ya kweli.