5 : 22
قَالُواْ يَٰمُوسَىٰٓ إِنَّ فِيهَا قَوۡمٗا جَبَّارِينَ وَإِنَّا لَن نَّدۡخُلَهَا حَتَّىٰ يَخۡرُجُواْ مِنۡهَا فَإِن يَخۡرُجُواْ مِنۡهَا فَإِنَّا دَٰخِلُونَ
Wakasema: Ewe Musa! Huko wako watu majabari. Nasi hatutaingia huko mpaka wao watoke humo. Wakitoka humo hapo tutaingia.
Explanation & meanings · 1
- Wana wa Israili wakaikhalifu amri ya Mwenyezi Mungu na wakasema: Ewe Musa! Katika nchi hii wamo watu majabari. Sisi hatuna nguvu za kupambana nao. Basi hatutoingia humo maadamu wao wamo. Wakitoka basi tena hapo sisi tutaingia.