Skip to content
Orodha ya Sura /

لُقمَان

لُقمَان is chapter 31 of the Quran and has 34 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

34 Aya Sura Na. 31
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

الٓمٓ

Alif Lam Mim (A.L.M.) .

Explanation & meanings · 1
  1. Harufi hizi zimeanzia baadhi ya Sura kuashiria kuwa Qur'ani ni muujiza ulio tungwa na harufi kama harufi wanazo zitumia Waarabu katika maneno yao. Na juu ya hayo wao wameshindwa kuleta mfano wake. Na pia ni kwa ajili ya kuzindua watu wasikilize na watege sikio. Na washirikina walikuwa wamewafikiana kuwa wawe wanaropokwa maneno ya upuuzi tu ikisomwa Qur'ani wala wasiisikilize.

تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱلۡكِتَٰبِ ٱلۡحَكِيمِ

Hizi ni Aya za Kitabu chenye hikima.

Explanation & meanings · 1
  1. Hizi Aya tukufu ni Aya za Qur'ani iliyo kusanya hikima na ukweli.

هُدٗى وَرَحۡمَةٗ لِّلۡمُحۡسِنِينَ

Kuwa ni Uwongofu na Rehema kwa wafanyao wema!

Explanation & meanings · 1
  1. Hizi Aya ni Uwongofu ulio kamilika, na Rehema iliyo kusanya kwa wenye kutenda mema.

ٱلَّذِينَ يُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُؤۡتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَهُم بِٱلۡأٓخِرَةِ هُمۡ يُوقِنُونَ

Wanao shika Swala, na wanatoa Zaka, nao wana yakini na Akhera.

Explanation & meanings · 1
  1. Hao ndio wanao timiza Swala kwa njia ya ukamilifu kabisa, na wanawapa Zaka wanao istahiki; na wao wanayaamini maisha ya Akhera kwa imani yenye nguvu kabisa.

أُوْلَٰٓئِكَ عَلَىٰ هُدٗى مِّن رَّبِّهِمۡۖ وَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ

Hao ndio walio na uwongofu utokao kwa Mola wao Mlezi, na hao ndio wenye kufanikiwa.

Explanation & meanings · 1
  1. Hao Waumini wanao tenda vyema vitendo vyao, wametua kwenye Uwongofu ulio wajia kutokana na Mola wao Mlezi. Na hao tu - si wengineo - ndio wenye kufuzu kikweli.