Skip to content
لُقمَان /

Aya 15

31 : 15

Aya 15 of لُقمَان (31 : 15). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

لُقمَان Aya 34
Sura · لُقمَان
Kiswahili · Barawani
31 : 15

وَإِن جَٰهَدَاكَ عَلَىٰٓ أَن تُشۡرِكَ بِي مَا لَيۡسَ لَكَ بِهِۦ عِلۡمٞ فَلَا تُطِعۡهُمَاۖ وَصَاحِبۡهُمَا فِي ٱلدُّنۡيَا مَعۡرُوفٗاۖ وَٱتَّبِعۡ سَبِيلَ مَنۡ أَنَابَ إِلَيَّۚ ثُمَّ إِلَيَّ مَرۡجِعُكُمۡ فَأُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ

Na pindi wakikushikilia kunishirikisha na ambayo huna ilimu nayo, basi usiwat'ii. Lakini kaa nao kwa wema duniani, nawe ishike njia ya anaye elekea kwangu. Kisha marejeo yenu ni kwangu Mimi, na Mimi nitakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda.

Explanation & meanings · 1
  1. Na ikiwa wazazi wako wakikushikilia kwa juhudi umshirikishe Mwenyezi Mungu na vitu usivyo vijua kuwa vinastahiki kuabudiwa, basi usiwakubalie. Lakini endelea na kusuhubiana nao duniani kwa wema na ihsani. Na fuata njia ya wanao rejea kwangu kwa Tawhidi, Imani ya Mwenyezi Mungu Mmoja, na Ikhlasi, usafi wa niya na vitendo. Kisha nyote mtarejea kwangu, na nitakupeni khabari ya mliyo kuwa mkiyatenda, ya kheri na shari, ili nipate kukulipeni kwayo.