31 : 21
وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱتَّبِعُواْ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ قَالُواْ بَلۡ نَتَّبِعُ مَا وَجَدۡنَا عَلَيۡهِ ءَابَآءَنَآۚ أَوَلَوۡ كَانَ ٱلشَّيۡطَٰنُ يَدۡعُوهُمۡ إِلَىٰ عَذَابِ ٱلسَّعِيرِ
Na wanapo ambiwa: Fuateni aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, husema: Bali tunafuata tuliyo wakuta nayo baba zetu. Je! Ijapo kuwa Shet'ani anawaita kwenye adhabu ya Moto uwakao?
Explanation & meanings · 1
- Na pindi wakiambiwa: Fuateni Haki na Uwongofu alio uteremsha Mwenyezi Mungu, wao husema: Bali sisi tunafuata tuliyo wakuta nao baba zetu. Je! Wanawafuata hao, ijapo kuwa Shetani ndio anawaitia wende kwenye upotovu utakao waingizia Motoni?