Skip to content
Orodha ya Sura /

السَّجدة

السَّجدة is chapter 32 of the Quran and has 30 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

30 Aya Sura Na. 32
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

الٓمٓ

Alif Lam Mim (A.L.M.) .

Explanation & meanings · 1
  1. Alif Lam Mim, ni harufi zilizo undiwa Qur'ani, kama yalivyo undiwa maneno yenu. Ikiwa mmeshindwa kuleta mfano wake hii, basi ni ushahidi kuwa hii inatokana na Mwenyezi Mungu, wala hakuisema mwanaadamu.

تَنزِيلُ ٱلۡكِتَٰبِ لَا رَيۡبَ فِيهِ مِن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Huu ni mteremsho wa Kitabu kisicho kuwa na shaka yoyote kinacho toka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Explanation & meanings · 1
  1. Huu ni uteremsho wa Qur'ani umetoka kwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote. Na Yeye ndiye mwenye kupanga mambo yao. Hapana shaka yoyote kuwa hii imeteremka kutoka kwake.

أَمۡ يَقُولُونَ ٱفۡتَرَىٰهُۚ بَلۡ هُوَ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّكَ لِتُنذِرَ قَوۡمٗا مَّآ أَتَىٰهُم مِّن نَّذِيرٖ مِّن قَبۡلِكَ لَعَلَّهُمۡ يَهۡتَدُونَ

Au wanasema: Amekizua? Bali hichi ni Kweli iliyo toka kwa Mola wako Mlezi ili uwaonye watu wasio fikiwa na mwonyaji kabla yako; huenda wakaongoka.

Explanation & meanings · 1
  1. Ati wanasema: Kaizua Muhammad, naye akamsingizia Mwenyezi Mungu! Haiwafalii wao kusema hayo. Kwani hii ni Haki, Kweli, iliyo teremka kutokana na Mola wako Mlezi, ili upate kuwakhofisha kwayo watu ambao hawajapata kujiwa na Mtume kabla yako, utaraji kwa onyo hili wapate kuongoka na waifuate Haki.

ٱللَّهُ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٖ ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰ عَلَى ٱلۡعَرۡشِۖ مَا لَكُم مِّن دُونِهِۦ مِن وَلِيّٖ وَلَا شَفِيعٍۚ أَفَلَا تَتَذَكَّرُونَ

Mwenyezi Mungu ndiye aliye umba mbingu na ardhi na viliomo baina yao kwa siku sita, na akatawala kwenye Kiti cha Enzi. Nyinyi hamna mlinzi wala mwombezi isipo kuwa Yeye tu. Basi, je, hamkumbuki?

Explanation & meanings · 1
  1. Mwenyezi Mungu aliye umba mbingu na ardhi na vilio baina yao kwa siku sita, kisha akatawala juu ya Kiti cha Enzi, A'rshi, kwa utawala ulio laiki naye. Nyinyi hamna badala yake Yeye yeyote msaidizi wa kukunusuruni, wala mwombezi wa kukuombeeni. Basi je, mtaendelea kushikilia kuwa katika ukafiri na inda, wala msiwaidhike kwa mawaidha ya Mwenyezi Mungu?

يُدَبِّرُ ٱلۡأَمۡرَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ إِلَى ٱلۡأَرۡضِ ثُمَّ يَعۡرُجُ إِلَيۡهِ فِي يَوۡمٖ كَانَ مِقۡدَارُهُۥٓ أَلۡفَ سَنَةٖ مِّمَّا تَعُدُّونَ

Anapitisha mambo yote yalio baina mbingu na ardhi, kisha yanapanda kwake kwa siku ambayo kipimo chake ni miaka elfu kwa mnavyo hisabu nyinyi.

Explanation & meanings · 1
  1. Yeye huyaendesha mambo ya uumbaji katika mbingu na ardhi, kisha amri yake hupanda kwenda kwake kwa siku ambayo kadiri yake ni kama miaka elfu kwa mujibu wa miaka ya duniani mnayo ihisabu nyinyi.