Skip to content
لُقمَان /

Aya 29

31 : 29
لُقمَان Aya 34
Sura · لُقمَان
Kiswahili · Barawani
31 : 29

أَلَمۡ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ يُولِجُ ٱلَّيۡلَ فِي ٱلنَّهَارِ وَيُولِجُ ٱلنَّهَارَ فِي ٱلَّيۡلِ وَسَخَّرَ ٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَۖ كُلّٞ يَجۡرِيٓ إِلَىٰٓ أَجَلٖ مُّسَمّٗى وَأَنَّ ٱللَّهَ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ

Kwani huoni kwamba Mwenyezi Mungu huuingiza usiku katika mchana, na huuingiza mchana katika usiku, na amedhalilisha jua na mwezi? Vyote hivyo vinakwenda mpaka wakati ulio wekwa. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.

Explanation & meanings · 1
  1. Je! Huangalii, ewe mwenye jukumu, kwa maangalio ya mwenye kuzingatia, ya kwamba hakika Mwenyezi Mungu huupunguza wakati wa usiku kwa kadri ya anavyo uongeza mchana? Na anaupunguza mchana kwa kadri ya anavyo uzidisha usiku? Naye amedhalilisha jua na mwezi kwa ajili ya maslaha yenu, na amefanya hayo yafuate mpango wa peke yao. Basi kila moja katika hayo huenda katika njia maalumu ya mbinguni wala haigeuki. Na mwendo huo unaendelea mpaka Siku ya Kiyama. Na hakika Yeye, Subhanahu, anazo khabari za yote myatendayo, na ni Mwenye kukulipeni kwayo.