Skip to content
Orodha ya Sura /

الهُمَزة

الهُمَزة is chapter 104 of the Quran and has 9 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

9 Aya Sura Na. 104
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

وَيۡلٞ لِّكُلِّ هُمَزَةٖ لُّمَزَةٍ

Ole wake kila safihi, msengenyaji!

Explanation & meanings · 1
  1. Atapata adhabu kali na maangamio huyo ambaye mtindo wake ni kuwafedhehi watu kwa kauli au kwa ishara, au kuwasengenya kuwavunjia hishima zao.

ٱلَّذِي جَمَعَ مَالٗا وَعَدَّدَهُۥ

Aliye kusanya mali na kuyahisabu.

Explanation & meanings · 1
  1. Ambaye amekusanya chungu ya mali na akawa kazi yake kuyahisabu tu, kwa kuona ladha huko kuhisabu.

يَحۡسَبُ أَنَّ مَالَهُۥٓ أَخۡلَدَهُۥ

Anadhani ya kuwa mali yake yatambakisha milele!

Explanation & meanings · 1
  1. Anadhani huyo kuwa mali yake yatamweka milele duniani, na yatamkinga na hayo anayo yachukia?

كَلَّاۖ لَيُنۢبَذَنَّ فِي ٱلۡحُطَمَةِ

Hasha! Atavurumishwa katika H'ut'ama.

Explanation & meanings · 1
  1. Na aache dhana hiyo! Wallahi! Hapana shaka yoyote kwa vitendo vyake viovu hivyo atakuja tumbukizwa katika Moto unao vuruga kila kinacho tupwa humo!

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡحُطَمَةُ

Na nani atakujuvya ni nini H'ut'ama?

Explanation & meanings · 1
  1. Na kitu gani kitacho kujuvya nini ukweli wa Moto huu wa H'ut'ama?