Skip to content
Orodha ya Sura /

الفِيل

الفِيل is chapter 105 of the Quran and has 5 verses. This page presents it in full in the Uthmani script, with a verse-by-verse translation of its meaning.

5 Aya Sura Na. 105
Nenda kwenye aya
Kiswahili · Barawani
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

أَلَمۡ تَرَ كَيۡفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِأَصۡحَٰبِ ٱلۡفِيلِ

Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo watenda wale wenye tembo?

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika, ewe Muhammad, unajua kwa ujuzi usio ingiliwa na shaka yoyote, alivyo fanya Mola wako Mlezi kuwafanyia wale watu wenye tembo (ndovu), wakataka kuishambulia Nyumba takatifu ya Al-Kaaba.

أَلَمۡ يَجۡعَلۡ كَيۡدَهُمۡ فِي تَضۡلِيلٖ

Kwani hakujaalia vitimbi vyao kuharibika?

Explanation & meanings · 1
  1. Unajua ya kwamba hakika Mwenyezi Mungu amejaalia juhudi yao kutaka kuibomoa Al-Kaaba ivize na ipotelee mbali. Juhudi yao ikapeperuka, na wao wasipate makusudio yao.

وَأَرۡسَلَ عَلَيۡهِمۡ طَيۡرًا أَبَابِيلَ

Na akawapelekea ndege makundi kwa makundi,

Explanation & meanings · 1
  1. Na Mwenyezi Mungu aliwasalitisha na majeshi ya ndege yaliyo watokea makundi kwa makundi yakifuatana, na yakawazunguka kila upande.

تَرۡمِيهِم بِحِجَارَةٖ مِّن سِجِّيلٖ

Wakiwatupia mawe ya udongo wa Motoni,

Explanation & meanings · 1
  1. Wakiwatupia mawe kutoka Jahannamu.

فَجَعَلَهُمۡ كَعَصۡفٖ مَّأۡكُولِۭ

Akawafanya kama majani yaliyo liwa!

Explanation & meanings · 1
  1. Akawafanya kama majani ya mimea yaliyo sibiwa yakatilifu.