Skip to content

Atayeapa kinyume na Mwenyezi Mungu basi atakuwa amekufuru au kafanya ushirikina

Imepokelewa Kutoka kwa bin Omar -Radhi za Allah ziwe juu yao- yakwamba yeye alimsikia mtu mmoja akisema: Hapana! naiapia Al-ka'aba, akasema bin Omar: Hakuapiwi kinyume na Mwenyezi Mungu, kwani mimi nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:

"Atayeapa kinyume na Mwenyezi Mungu basi atakuwa amekufuru au kafanya ushirikina"

«مَنْ حَلَفَ بِغَيْرِ اللهِ فَقَدْ كَفَرَ أَوْ أَشْرَكَ».

Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Ahmad
Sahihi
Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayeapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu na majina yake na sifa zake basi atakuwa kamkufuru Mwenyezi Mungu au kafanya ushirikina; kwa sababu kiapo humaanisha kutukuzwa mwenye kuapiwa, na utukufu ni wa Allah pekee; hakuapiwi ila kwa Allah na majina yake na sifa zake kutakasika machafu ni kwake. Na kiapo hiki ni katika shirki ndogo; lakini ikiwa muapaji atakitukuza alichokiapia kama anavyomtukuza Allah Mtukufu au zaidi; basi hapo itakuwa katika ushirikina mkubwa.

Maana ya Maneno

من حلف: الحلف: اليمين، وهي توكيد الحكم بذكر معظّم تطمئن له نفس المخاطب.

كفر أو أشرك: يحتمل أن يكون هذا شكًّا من الراوي، ويحتمل أن تكون "أو" بمعنى الواو فيكون كفر وأشرك.

Katika Faida za Hadithi

Nikuwa kutukuza kwa kiapo ni katika haki za Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka- hakuapiwi ila kwa Allah na majina yake na sifa zake.

Pupa ya Masahaba katika kuamrisha mema na kukataza maovu, hasa hasa uovu unapokuwa unahusiana na ushirikina mkubwa au kufuru.

Rejea

Sunanu Tirmidhiy (3/ 194) (1535).

Sunanu Abii Daud (5/ 154- 155) (3251).

Musnad wa Ahmad (9/ 249) (5346).

(9/ 275) (5375).

(10/ 249) (6072).

(1/ 343).

Zaidi (11)

فتح المجيد شرح كتاب التوحيد.

لعبد الرحمن التميمي (ص413).

القول المفيد على كتاب التوحيد.

لابن عثيمين (2/ 214).

الملخص في شرح كتاب التوحيد.

لصالح الفوزان (ص326).

الجديد في شرح كتاب التوحيد.

لمحمد القرعاوي (ص365).

التمهيد لشرح كتاب التوحيد.

لصالح آل الشيخ (ص452).

فتاوى اللجنة الدائمة.